UKIONA DALILI HIZI UJUE MUDA SI MREFU HUTAKUWA MWENZETU UNAENDA LEVEL NYINGINE.


1. Unaletewa kadi nyingi za mialiko hadi unasikia kero sijui kwenye kamati,ugeni maalumu,rasmi n.k.....Hupaswi kujisikia kero wewe changia hizo kadi hata kama hutapata muda wa kushiriki. Hao wanakuandalia mazingira ya kuinuliwa kwako na unachopanda kwenye hizo kadi utajitengenezea urahisi wa kufika kwenye hatma yako.

2. Kila tatizo likitokea nyumbani unapigiwa simu wewe,mama au baba kuumwa, hela ya kununua mbegu za shambani wewe, kukarabati nyumba hakuna ndugu anayehamasika ila mzigo huo unao wewe,,,,,kuna wakati unaona kama una majukumu mazito yasiyokuhusu......Hutakiwi kukasirika Fanya hayo kwa amani, muda si mrefu unaenda kuwa mtu asiye wa kawaida.

3. Kuongea na mtu kwenye simu zaidi ya dakika 10 hasa mambo yasiyo na maana kama salamu,stori, automatic unajiona unapoteza muda maana muda ni Mali, au unapenda short sms sio message kurasa tatu.....ujue upo karibu na lango la mafanikio.

4. Unaanza kuona masaa yanasogea sana,unajaribu kukimbizana nayo lkn bado unakuta majukumu ni mengi kuliko muda, ujue wewe ni level nyingine.

5. Unawahi sana kuamka na kuechelewa kulala.

6. Kila ukikaa ukitazama miaka yako unaona ndoto yako imechelewa sana.....na hautaridhika....yaani ndani yako unakumbwa na mahangaiko fulani lakn yasiyokuletea msongo wa mawazo unaosababisha vidonda vya tumbo......ila kutokutulia kwako kunakuletea utulivu ktk roho yako.

7. Utaona unakula kwa kiasi , unachagua chakula, si kwasababu vingine vinakudhuru ila ni kawaida mwili utakuwa unachambua vyakula.....unatembea kwa kiasi, muda mwingi unasoma na kuandika ili kutunza kumbukumbu.

8. Kama Ulikuwa na asili ya kuongea ongea ovyo bila kiasi..utaona hauongei na hujatega sikio lako kusikiliza fulani kasema nini.... .

9. Kuna aina ya Marafiki wasio na msaada kwako hutatumia nguvu kubwa kujitenga nao ila ni automatically watajitenga nawe hata bila kukosana.

10. Hutakuwa na watu uliowabeba moyoni na ukawa na uchungu nao.....maana yake ni kwamba, ikiwa una sura za watu waliowahi kukuumiza,unatembea nao,unalala nao hata kuwaota,na unawaombea mabaya pengine, ujue bado sana kufika unapotakiwa ufike....utachelewa sana. Lkn mtu wa kuinuliwa ana msamaha mkubwa sana,ni mpuuziaji wa taarifa mbaya za kumjeruhi.

11. Ndoto unazoota upo na wakuu wa nchi au viongozi wa Imani.....ujue muda si mrefu utaenda kutolewa ulipo na kuketishwa na wakuu.

12. Utaona hali ya utoaji inaongezeka.....yaani unatoa kwa hiari, unasikia usanehe baadhi ya madeni kuwatoa watu ktk kifungo cha madeni.....ule ubahiri uliokuwa nao hadi wazazi wako wanakujua wewe ni bahiri utaondoka....unakuwa ni mtu wa kutoa misaada kulingana na kipato chako hata bila kuombwa.

13. Kuna wakati unafua nguo unakuta ulishasahau elfu 5 au 10 au elfu 20, sio uzembe au kutokuwa na nidhamu ya hela ila ni kwasababu unaenda kuinuliwa.

Sio mwanamke anafua nguo hata 200 haikuti! anakutana na leso za mafua tu zimejaa kamasi😐sio kosa lako ila majira yako bado😊

14. Unaanza kufurahia kutembelewa na wageni, hiyo haijalishi unavyo au huna,ila unakuta unajisikia amani ukiwa na wageni.....ujue unakaribia kuinuliwa maana hakuna mkaribisha wageni amvaye akabaki hatua ile ile.

15. kuna hali kwako itabadirika,kama kuombaomba kujipunguzia vitu utaanza kuona aibu! kuna maeneo ulikuwa unakaa utaanza kuona hutakiwi kukaa huko maana sio wa level ya huko .

Post a Comment

0 Comments