Sote tunapaswa kuishi kwa Imani ....
Tunaishi kwa imani na si kwa kuona (3 Wakorintho 5:7)
Imani inatokana na kuusikia ujumbe, na huo ujumbe unatokana na neno la Kristo (Warumi 10:17)
Kuwa na imani ni kuwa na hakika ya mambo tunayotumainia; kusadiki kabisa mambo tusiyo yaona. Maana wazee wa kale walipata kibali cha Mungu kwa sababu ya Imani yao. (Waebrania 11:1-)
Maandiko yanasema; lakini mwadilifu wangu ataishi kwa imaniwalakini akirudi nyuma, mimi sitapendezwa naye (Waebrania 10:38)
Kwa Imani Abrahamu alimtii Mungu alipoitwa aende Katika nchi ambayo Mungu Angempa iwe yake (Waebrania 11:8)
Yesu alisema mambo yote yawezekana kwa mtu aliye na imani (Mark 9:23). Kwa imani Sarai aliamini kwamba Mungu hutimiza ahadi zake akaweza kubeba mimba ijapo umri wake ulikuwa umeenda sana (Waebrania 11:11)
Na sasa naishi, lakini si mimi tena, bali Kristo anaishi ndani yangu. Maisha haya ninayoishi sasa naishi kwa Imani, imani Katika Mwana wa Mungu aliyenipenda hata akayatoa maisha yake kwa ajili yangu. (Wagalatia 2:20)
Basi Mpendwa, mtumainie Mungu kwa moyo wako wote wala usitegemee akili zako mwenyewe (Methali 3:5-6). Maana mwenye kutawaliwa na fikra za mwili ni adui wa Mungu .... watu wanaotii matakwa ya mwili hawawezi kumpendeza Mungu (Warumi 8:7)
Kutokana na hayo Tuseme nini zaidi? Ikiwa Mungu yuko upande wetu nani awezaye kutupinga? (Warumi 8:31)
0 Comments