MPANGO WA MUNGU WA KWANZA KATIKA FAMILIA

Karibuni wapendwa wangu katika wilnismstore library ya maarifa ya kiimani, leo nimewaandalia Makala hii nzuri ambayo inaangazia mpango wa Mungu kwanza katika familia kama una lelote la kuongezea basi shuka hadi sehemu ya comments kisha niandikie

Songa nayo.....

Familia ya kwanza imeanzia katika bustani ya Edeni na muasisi wa familia ni Mungu mwenyewe kwa mujibu wa maandiko Matakatifu Mwanzo 1:26 Mungu akasema natumfanye mtu kwa mfano wetu,kwa sura yetu wakatawale samaki wa baharini na ndege wa angani na wanyama na nchi yote pia na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.

Hapa tunaona mambo yafuatayo:

Mwanadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu kwa maana nyingine Mungu alikusudia huyu mwanadamu afanane naye.

Mwanadamu anaumbwa akiwa na sura ya Muumba wake hapa inaleta tofauti kubwa kati ya mwanadamu na viumbe wengine sisi tumeumbwa kwa sura ya Mungu na hii ni habari njema kwa watu wote.

Mungu anawapa mamlaka ya kutawala viumbe wote wa nchi kavu baharini na angani haya ni mamlaka kubwa sana hivyo sisi ni watawala wa viumbe wote.

Hii ni sehemu ya kwanza ambayo kila mwanafamilia anapaswa kuifamu anapokuwa katika familia yake kuwa yeye ni mtawala hivyo maisha yake anayoishi aishi kama mtawala anayemuwakilisha Mungu hapa duniani.


Mwanzo 1:27 Mungu akamuumba mtu kwa mfano wake kwa mfano wa Mungu alimuumba mwanaume na mwanamke aliwaumba.
Mwanzo 1:28 Mungu akawabariki Mungu akawaambia zaeni mkaongezeke mkaijaze nchi na kuitiisha mkatawale samaki wa baharini na ndege wa angani na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi

Hapa Mungu anawapatia Baraka za kuzaa kuongezeka na kuijaza nchi hivyo watoto ni mbaraka kutoka kwa Mungu inapaswa wanafamilia kujua kua mbaraka huu unatokana na Mungu mwenyewe na sio mapenzi ya mwanadamu hivyo watoto wanapokuwepo katika familia waonekane kama mbaraka na familia ambayo haijapata watoto waendelee kumuomba Mungu yeye ni muaminifu atawapatia kwa majira mbaraka huu.

Mwanzo 2:18 Bwana Mungu akasema sii vyema huyu mtu awe peke yake nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.
Mwanzo 2:21 Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito naye akalala kisha akatwaa ubavu wake mmoja akafunika nyama mahali pake.Na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke akamleta kwa Adamu.
Mwanzo 2:23 Adamu akasema huyu ni mifupa kaika mifupa yangu na nyama katika nyama yangu basi ataitwa mwanamke kwa maana ametwaliwa katika mwanaume.

Mungu anaona sio vyema Adamu awe pekee yake hivyo anamfanyia msaidizi wa kufanana naye

KUFANYIWA:
Anayemfanya mwanamke ni Mungu mwenyewe hivyo ili kuwa na familia bora kila anayetaka kuingia katika familia anapaswa kumuomba Mungu Mke mwema au Mume Mwema

Hapa tunaona neno msaidizi:
Mwanamke hapa anatajwa kama msaidizi wa mwanamume hivyo kila mwanaume anapaswa kujua kua mwanamke ni msaidizi wake hapaswi kuachiwa majukumu ya familia

Neno la mwisho hapa ni wa kufanana naye:
Mwanamke amefanana na mwanaume hivyo kila anachofikiri kufanyiwa mtu mke au mume ndicho amfanyie mwenzake akikumbuka wamefanana.

> Mwanamke ametoka katika sehemu ya mwanaume hivyo wanapaswa waishi kwa kupendana na kuheshimiana wao ni mwili mmoja.

●Huu ndio mwanzo wa familia kabla ya dhambi 
●Mungu alikusudia familia hizi kuwa njema sana zikiitangaza tabia yake katika ulimwengu huu

Mungu atupatie wepesi wa kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika familia zetu, atufundishe kuishi kwa mapendo na kukumbuka ahadi na viapo vyetu vya  ndoa.

Ahsante sana na Mungu akubariki kwa kuisoma hii Makala, endelea kufuatilia Makala zetu na utajifunza mengi zaidi, kama una ushauri niandikie sehemu ya comments hapo chini


Andika comment yako hapa

Post a Comment

5 Comments

Emoji
(y)
:)
:(
hihi
:-)
:D
=D
:-d
;(
;-(
@-)
:P
:o
:>)
(o)
:p
(p)
:-s
(m)
8-)
:-t
:-b
b-(
:-#
=p~
x-)
(k)