MAFUNZO YA NDOA
Wanaume Wenzangu Naomba Mnisikilize kwa Umakini.
Hivi mke wako Anawezaje Kuwa sawa Na Mchepuko wako ? Au wakati mwingine Unasema Mkeo Sio mrembo kama mchepuko wako kwanini lakini ?
Embu Angalia, umempa ujauzito mara 3 au 4 wengine mpaka mara 6. Ameingia Leba kukuzalia watoto mara zote hizo.
Mkeo anapitia taabu nyingi wakati anapokuwa mjamzito, wakati mwingi analala upande upande kwa sababu ya kiumbe chako kilichokuwa tumboni mwake.
Akisha jifungua anapambana kunyonyesha na kukulelea watoto wako mpaka wanafikia umri wa kuondoka nyumbani, anakupikia , anakufulia na kukufanyia shuhuli zote za nyumban je mchepuko wako angeweza yote hayo ??
Mara nyingi mke wako amelazwa hospitali kwa ajili ya watoto wako lakini bado yupo ngangari anapambana.
Wakati mwingine Amechanwa tumbo lake kwa kushindwa kujifungua kwa njia ya kawaida lakini yeye bado yupo sawa anatabasamu siku zote.
KNOW MORE ABOUT US>>>
Ulimchukua mtoto wa watu ngozi nyororo , na bado mrembo lakini kutokana na kukubebea wanao na kukulelea kwa kuwanyonyesha maziwa yake yamelala, amepata michirizi isiyoisha katika tumbo lake yote sababu yako na wanao.
Wakati alipokuwa mjamzito alishindwa kula, mara nyingi alikuwa anatapika, umemchukua mtoto wa watu unamfungia ndani haruhusiwi hata kufanya kazi maana ulimwachisha ili awe wa kukulea wewe na watoto wako. Lakini bado unashindwa kumuheshimu.
Embu Mchukue Mchepuko wako Umuweke katika Hii Safari ambayo mke wako amepitia na bado anaipitia uone kama ataweza kuifanya kwa ubora kama mke wako.
Niwaombe tu Kaka Na Ndugu Zangu. Jifunzeni Kuwaheshimu na Kuwapenda Wake zenu. Jaribuni kukumbuka kwamba ni kwa sababu yetu wanaume wanawake wanapitia Dhahama zote hizo.
NAWAPENDA.
0 Comments