FAHAMU NGUVU YA MTU MMOJA TUU



Yeremia 5:1

Pigeni mbio huku na huku katika njia za Yerusalemu, mkaone sasa, na kujua, na kutafuta katika viwanja vyake, kwamba mwaweza kumpata mtu mmoja, kwamba yuko mtu mmoja awaye yote atendaye kwa haki, atafutaye uaminifu;nami nitausamehe mji huo.


Ezekieli 22:30

Nami nikatafuta mtu miongoni mwao,atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu._

"SIKIA!"

Mpenzi msomaji, palipo na wengi pana faida, nguvu na hata ushindi mkubwa. Lakini yanini kuhangaika kutafuta tafuta watu wengi wakati ukuta wangu umebomoka na ni wewe tu uliyepewa kuona, na hata hakuna mwingine atiaye nia katika haki ili kuujenga pia.

Mimi sikusema kuwa; "nalitafuta mtu mmoja tu anipendezaye na kwenda katika njia zangu nami nitauponya mji?"

Kwa mtu mmoja, dhambi iliingia ulimwenguni na kuleta mauti. Na kwa mtu mmoja msamaha ulifikilia, na dhambi iliondoka ulimwenguni na kuleta haki. Na kwa ufunuo wa mtu mmoja, nikalijenga kanisa langu la kwanza na mauti na kuzimu haikuliweza.Je, unajua nguvu ya mtu mmoja katika kuujenga au hata kuubomoa mji?

Nimekuangalia wewe tu, na nimekuamini wewe tu, kuwa waweza simama katika boma lililobomoka na kulijenga ili nipate kuponya nchi.

Wewe u rungu langu, wewe u silaha yangu ya vita. Na kwa wewe, nitaweza haribu au kutengeneza, bomoa au kujenga, kung'oa au kupanda.Wewe peke yako ni zaidi ya unavyojifikiria.  Fungua macho yako uone sasa ukubwa na nguvu kuu niliyoiweka ndani yako; utahamisha milima.

Usipapase papase na kutafuta tafuta kujua utakuwa na nani katika kujenga mji. Tia nia kwa dhati kisha utawaona wasaidizi wenzako wakija kujiunga nawe katika ujenzi wa hekalu langu.

Naam! Kusanya mchanga, weka kokoto, tia simenti, weka maji, changanya zege.Naam; wapo watakaoubeba mchanganyo huo na kuufikisha katika msingi uliowekwa tayari kabisa na kumimina kwa ujenzi. Usipofanya hayo tayari, hutawaona wabebaji na wajengaji wakija pamoja nawe ili kukusidia. Kwa maana walio upande wako ni wengi kuliko walio katika upande wa uharibifu. Jenga kwa hekima tu na epuka kelele.

NALITAFUTA MTU MMOJA TU NITAKAYE JIDHIHIRISHA KWA ULIMWENGU KUPITIA YEYE. MTU MMOJA TU, KAMA ISHARA KWA TAIFA NA MATAIFA KUWA: "MIMI NIKO AMBAYE NIKO, HATA MILELE."NA KWA YEYE NITALIJENGA BOMA LANGU TENA LILILOANGUKA NA KUBOMOKA. "MTU MMOJA TU, NAMI NITAONEKANA!"

(Mimi ni Mungu; Bwana, katika Roho Mtakatifu, nitoaye taarifa kabla hayajakuwako.)

BARIKIWA!

Soma zaidi....
💡 Wakolosai 4:5 🏃🏾‍♂️


Andika maoni yako hapa

Post a Comment

1 Comments

Emoji
(y)
:)
:(
hihi
:-)
:D
=D
:-d
;(
;-(
@-)
:P
:o
:>)
(o)
:p
(p)
:-s
(m)
8-)
:-t
:-b
b-(
:-#
=p~
x-)
(k)