“Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika, ni heri mwanamume asimguse mwanamke. Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe. Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake. Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe.”
Tumsifu Yesu Kristu,
Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu,
Leo kuna ujumbe wa wanandoa, wanandoa tunawaona na tunakutana nao kila siku, na matatizo yao tunayaona kila siku na imefikia wengine kusema kama ndoa zenyewe ndio hivi ni heri nisioe au nisiolewe,yote hii nikutokana na vile wanandoa wanaishi,
Imeandikwa Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi (Waebrania 13:4) lakini ndoa nyingi zemekua nichafu na zinanuka, kila iitwapo leo aman, uchungu vinyongo kwenye ndoa vinazuka na kushamili, mume kukimbia familia nikitu kilichofanywa kuwa kawaida sana katika ndoa, wanaume sasa hivi kumkimbia mke ndio imekua fashion sasa sijua kuwa hawajaelewa maana ya agano au vipi maana unapoapa mbele ya madhabahu maana yake umejifunga na Mungu kuwa utamtunza na kuishi na mke mmoja milele au kuishi na mume mmoja milele, badala yake mume anakua na vidumu nje,anatembea na makahaba nje matokeo yake wanaume wanawahi kufa na kuacha rundo la wajane maana ukivunja agano na usipotubu kifo lazima kikutokee tu.
Ikiwa kunatatizo katika ndoa mnakaa mnatafuta njia ya kulimaliza tatzo sio kukimbia tatizo na kuacha watoto wanateseka kwani hakika nawaambia mtadaiwa mbele za Mungu maana mmewazaa watoto kwa pamoja ili muwatunze muwalee pamoja na muwatunze pamoja sio uzalishe harafu ukimbie majukumu haipo hivyo, jishushe tu ili utatue matatizo ndoa ipate kuwa na furaha, Na baba wewe ndio kichwa cha familia na unatakiwa uwe kiongozi wa familia maana yake panapo tokea tatizo kwenye familia wewe ndio unatakiwa usimame imara katika kutatua matatizo imeandikwa ishini na wake zenu kwa akili (1Petro3:7), pia imeandikwa jua lisichwe ukiwa na hasira moyon maana yake zaidi ya hapo unapolala na hasira dhambi ni yakwako, na dhambi ikizaa mwisho ni mauti sasa unajua ni lini utakufa? je ukilala na hasira + uchungu harafu usiku ukifa je utakua mgeni wa nani mbinguni, mwana ndoa kubali kuachilia, achilia roho ya msamaha ndani yako ili anano la ndoa lipate kutimilika.
Acha roho ngumu, humkomoi mtu bali unajikomoa mwenyewe, lazima wanandoa ili kuepusha kizazi cha laana, mikosi na magumu kwa watoto wao lazima wasolve matatizo yanayotokea katika ndoa (Kutoka 20:5),na kupitia hivyo ndoa zitakua taasisi ya Mungu yakuzalisha watumishi wakubwa na wakuupindua ulimwengu.
Wake katika ndoa ndio kiwili wili, sasa wake kuna nyakati wanazizoea ndoa kiasi wanapelekea kutofanya majukumu yao kwa ufanisi, wengine wanataka nao waonekane wanajua kuongea kila kitu ambapo mume akifoka na yeye anamfokea mumewe, hata siku moja mafahari wawili hawakai zizi moja kwenye ndoa ikitokea magonvi wote wanapanda hakutakua na maelewano, ila mmoja akipanda mwingine akishuka ndoa aman inakuja na ndoa inasonga mbele.
Kinachochangia pia ndoa kuwa na migogoro mikubwa ni kutokua na ibada, kwenye ibada ndiko kwenye tafakari mbalimbali ambazo zinaleta kujua Mungu anataka nini na hataki nin, ibada inapokosekana kwenye ndoa adui anapata mlango wa kuingia na kuipiga ndoa mwisho wake ndoa ilikua imara magonvi yanakua hayaishi na mwisho inaishia kuachana na hapo mume anaenda kuoa mke mwingine na kuolewa na mume mwingine ambapo inakua kinyume cha agano waliloweka madhabahuni usidanganyike malipo ya kuvunja agano utayapata hapa hapa dunian, weka utaratibu wa maombi ndani ya nyumba kila siku, tafakari ya Neno ikijaa kwenye familia Yesu anakaa ndani ya familia hivyo adui hata akija anakosa pakushika maana ule ulinzi wa Mungu juu yetu kwa Iman unafanya kazi.
Kijana ambae bado hujaolewa tulia mngoje Bwana omba umpate wakuoa au kuolewa nae alie sahihi, usijichafue kwa kufunua sketi na kufunuliwa sketi zako unamuhuzunisha na kumpoteza Roho mtakatifu ndani yako. Tafuta kujenga jamii ya baraka na ndoa ya baraka kwa kujitunza na kuiheshimu ndoa yako,
Wewe ambae unaona muda umepita wa kuolewa au kuoa usiruhusu mawazo ya kuzaa pasipo na ndoa, usiruhusu kuolewa na mtu wa mataifa, usiruhusu kuolewa na asie mkristo mngoje Bwana atakupa wa kwako alie mzuri. Kwani anakuwazia mawazo yaliyo mema (Yeremia 29:11), zidi kujitunza ukiona unaishiwa nguvu omba Mungu akutie nguvu uweze kuishinda roho ya kuanguka, omba Roho ya uvumilivu uweze kuvumilia yote katika yote kabla na baada ya ndoa.
Ushindi wa ndoa yako ni Maombi tu, hata ndoa ikiwa chungu vipi hilo ni agano mwambie Bwana Yesu amtengeneze huyo mwanandoa mwenzio chochote usichokipenda kwenye ndoa omba kwa bidii na kwa Iman acha kukata tamaa, ndoa sio mateso ndoa ni Furaha, ondoa kisilan moyon juu ya mkeo au mumeo kwa yote aliyokukosea, msamehe hata kama moyo ulivunjika, ita nguvu za Mungu ndani yako, hata ukichukia milele haisadii Bali tangaza msamaha ili ndoa ibarikiwe,
Let your Faith move the mountain and don’t allow the mountain to belittle your Faith..!!
God gives you as much wisdom as you ask Him for, only do not doubt, for you will get nothing..!
"If any of you needs wisdom to know what you should do, you should ask God, and he will give it to you. God is generous to everyone and doesn’t find fault with them. When you ask for something, don’t have any doubts. A person who has doubts is like a wave that is blown by the wind and tossed by the sea. A person who has doubts shouldn’t expect to receive anything from the Lord. A person who has doubts is thinking about two different things at the same time and can’t make up his mind about anything...."
0 Comments