Ndugu tunaposoma katika injili ya (mathayo6:1),
"Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu,kusudi mtazamwe na wao kwa maana mkifanya hivyo hampati thawabu kwa baba yenu alie mbinguni(Mungu)
Watu tulio wengi tunavaa maisha yasio uhalisia ili tuonekane kwa nje kuwa ni wema ila ndani hatupo hivyo.Tuishi maisha yetu,tusijifanye wema kumbe ndani tumejaa umbea,unafiki,chuki,masengenyo,uuaji,uzinzi, kiburi na mambo Mengine maovu ambayo uhalisia wa nje huyaficha.Tunapofanya hivyo tujue hakuna kinachofichika machoni pa Mungu.Yeye ajua yote,hata mawazo yetu( CFR.katekisimu yetu (katoliki) pp1-2)
Sasa tujiulize tulio wakristo kuwa ukristo wetu ni kitu gani na unanafasi gani katika maisha yetu ya uhalisia ya kila siku?Je,ubatizo tu unatosha Mimi kuwa mkristo?
Jibu ni hapana,kuwa mkristo ni kuwa karibu na kristo,kuwa rafiki ya kristo,kufanya Yale Kristo alotuagiza kutenda,kumpenda Mungu na Jirani(Marko 12:29)kupendana kama vile yeye alivyotupenda(alhamisi kuu alipoweka amri ya upendo-amri mpya)
Maana penye upendo ipo Amani,ipo furaha,kupo kujuliana,kuvumiliana na wala hapana unafiki,wala chuki,wala magomvi wala marumbano.
Kila mkristo anatakiwa aishi ukristo wake.mlei atimize wajibu wake wa kilei,mtawa vivyo hivyo na kasisi kwa namna ya pekee afanye impasavyo kutenda.maana wito alionao kila mmoja wetu ameuitikia mwenyewe tena kwa hiyari.
Unafiki hufanya hata wengine wapoteze imani yao.Kusema wew ni mkristo na kutokuishi ukristo huo ni unafiki.Kuishi maisha ya kinafiki ni kuishi umbea.Kristo anasema "Hao wamekwisha pata thawabu yao Bali wewe. .."
Mbingu ipo karibu nasi kama tutatenda itupasavyo na iko mbali kama tutatenda kinyume na maisha tuliojichagulia kuishi yaani ukristo katika ulei,utawa na hata ukasisi.
Kwa kifupi kujifanya wewe ni kondoo kumbe mbuzi haisaidii hata kama mnaishi zizi moja.usiishi maisha ya mtu mwwngine ili watu wakuone mwema kumbe lah!ishi maisha yako ili ukosolewe.
Wakati Fulani mfanya biashara mmoja wa matunda aina ya machungwa alianzisha kijiwe sokoni.akawa anauza machungwa kwa wingi maana alikuwa anajua kiingereza hivyo wateja wake wengi walikuwa wazungu.Basi alizoea wale watu wakija huwa wanashika machungwa huku wanamuuliza " how much shillings"
Yeye huwa anawajibu " one hundred,two hundred and five hundred.
Tena huwa wanamuuliza "are they sweetable"
Yeye huwajibu "sometimes yes but sometimes no"
Basi jirani yake kulikuwa na mfanya biashara mwengine ambaye naye alikuwa akiuza machungwa.Alikuwa akiumia moyoni kutokana na mwenzake kuuza sana hivyo naye alitamani kuwa kama rafiki ake hivyo alikuwa anamsikuliza wakiwa wanaongea ila kwa bahati mbaya hakuwa anajua kiingereza.Basi alomeza baadhi ya majibu tu.
Siku moja yule mfanya biashara alikuwa ametoka Basi wale wazungu wakaja na walipofika hawakumkuta hivyo yule rafiki mfanya biashara akaona ule ndio wakati wa kuwateka wale wazungu.Basi wale wazungu huku wanashikashika machungwa ya yule jamaa wakamuuliza
"Where is my friend" jamaa akakurupuka one hundred,two hundred and five hundred akijua kama ameulizwa kuwa machungwa ni shilingi ngapi kumbe sio.Mzungu akashangaa akamuuliza "are you crazy" akajibu sometimes yes but sometimes no.Basi mzungu akaondoka akijua kuwa yule mtu ni chizi.
Alijishushia hadhi kwa kutaka kuishi maisha ya wengine Basi tuombe neema ya Mungu ili atujalie kila mmoja kwa wito wake aishi maisha ya uhalisia aliochagua,tuwe chumvi kwa jamii,tuwe mwanga,tuwe kioo kwelikweli tukionesha picha halisi ya Kristo mfufuka.Tuachane na chuki,masengenyo nk kwani hayo sio maisha ya kikristo .Tuishi ukristo vizuri ili tufikie ule wito mkuu tuloitiwa yaani kuwa watakatifu.
Tumsifu Yesu Kristo,
0 Comments