FAHAMU NI JINSI GANI SOCIAL MEDIA INAWEZA KUUWA MAISHA YAKO YA KIROHO


Social media inaweza kukuharibia mahusiano yako na Mungu usipokuwa makini na shetani anaweza kutumika mlango huu kukuvuta mbali na Mungu badaya ya kutumia mda mwingi Kutafakari na kusoma Neno la Mungu unajikuta asubuhi mpaka jioni busy na social media kiasi kwamba hata ile fellowship na Mungu inapotea.
Internet, Magaeti,Tv, simu n.k tunapaswa tutumie kwa kiasi. Tusipokuwa makini tutajikuta muda wote tunautumia kwa kuchat, mtu ataanzia facebook, anaenda Instagram, baadaye Twitter kisha Snapchat, WhatsApp, Telegram, IMO, Wechat, Palmchat n.k hadi anakuja kumaliza kutembelea mitandao hiyo yote tayari siku imepita.

Mwingine yeye ni kuangalia runinga tu, anatoka chaneli hii anaenda ile au unakuta yeye ni mtu wa kubadili CD tu na hizi season ndio zimewamaliza kabisaaa.

Hebu tuwe na muda maalum wa kuwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii pia.

Mitandao ya kijamii inaweza kuwa na faida na madhara. Baadhi ya Wakristo wamechagua kutotumia mitandao ya kijamii. Wakristo wengine hutumia mitandao ya kijamii kuwasiliana na watu wa familia na marafiki. Hata hivyo, Ibilisi naye anataka tutumie mitandao ya kijamii kwa njia isiyo na hekima, na hilo litaharibu sifa yetu na hali yetu ya kiroho. Kama Yesu, tunaweza kutumia  Neno la Mungu ili kutambua na kuepuka hatari. (Lu 4:4, 8, 12)

MAMBO YA KUEPUKA WAKATI WA KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII:

  • Kutumia mitandao ya kijamii kupita kiasi. Kutumia mitandao ya kijamii kwa saa nyingi kunaweza kutunyima wakati wenye thamani tunaohitaji ili kufanya mambo ya kiroho(Efe 5:15, 16; Flp 1:10)
  • Kutazama mambo yasiyofaa. Kutazama picha zisizofaa kunaweza kutufanya tuwe waraibu wa ponografia au kujihusisha katika maadili mapotovu. Kusoma habari za waasi-imani kunaweza kuharibu imani ya mtu (Mt 5:28; Flp 4:8)
  • Kuweka picha au maelezo yasiyofaa. Kwa kuwa moyo ni wenye hila, huenda mtu akawa na mwelekeo wa kuweka picha au maelezo yasiyofaa kwenye mtandao wa kijamii. Hata hivyo, hilo linaweza kuharibu sifa ya mtu au kudhoofisha imani yake( 14:13; Efe 4:29)

KUMBUKA
Mungu amekuweka hapa duniani kwa makusudi tafuta kujua kusudi la Mungu juu ya maisha yako. Mkaribieni Mungu naye atawakaribia. Unapokuwa karibu na Mungu ndipo anapoanza kukufunulia siri za ufalme wake. Kwa hiyo kazi kubwa ya shetani ni kukutenga mbali na Mungu ( kumbuka mkimbieni shetani naye atawakimbia )

Yakobo 4:7-8
Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.
Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.
Hiyo ni mbinu kubwa ya shetani pata kuelewa fikra zake juu ya maisha yako.

2 Wakorintho 2:11
Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake.
Tifike mahali tujipime upendo wetu juu ya Mungu. tunapokiri tunampenda Mungu je ni vitu gani vimeteka muda wetu? Au vipaumbele vyetu viko kwenye nini??

Yohana 14:23-24
Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.
Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; .....

Mathayo 15:8
Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami.

1 Yohana 2:15,17
Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.
Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.

Ufunuo wa Yohana 2:5,7
Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.
Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu.


Andika comment yako hapa

Post a Comment

0 Comments