TAFAKARI KUHUSU MSALABA WA BWANA

"Lakini mimi, hasha nisione fahari juu ya kitu chochote ila msalaba wa Bwana, ambao kwa huo ulimwengu umesulibishwa kwangu" (Gal 6:14)

Kimsingi maisha au athari za msalaba wa Bwana haziepukiki kwa mfuasi wa Kristo katika maisha ya kila siku ili kupata wokovu.

Ni maisha yanayodai sana utii na uaminifu katika kutimiza mapenzi ya Mungu kwani yeye alitii hata kufa msalabani ili atukumboe sisi.
(Filp 2:6-11)


Msalaba hutufanya  kuwa na tamaa takatifu ya  maisha ya mbinguni kama yule mwizi aliyetubu: "Bwana unikumbuke katika Ufalme wako.... Utakua pamoja nami leo Paradisini" (Lk 23:42,43). Heri wafao mikononi mwa Bwana maana wataishi naye milele.


Msalaba hutukumbusha wajibu wa kifamilia katika kuhudumiana: Mama tazama mwanao, mwana tazama mama yako (Yn 19:26, 27)


Msalaba hutupa kiu ya daima ya kumtafuta Mungu mkombozi na mwokozi aliye Maji ya uzima wetu : "Nina kiu" (Yn 19:28). Ikoleze kiu yako ya kumuona Mungu kwa matendo mema.


Msalaba huzisalimisha na kuzikumbatia roho zetu katika mikono salama ya Mungu: "Baba mikononi mwako naiweka roho yangu." (Lk 23:46).kabidhi maisha yako kwake na si malimwengu.


Msalaba ni kielelezo cha udhaifu wetu wa daima unaokamilishwa na nguvu ya Mungu tu na pasipo yeye hatuwezi kitu:  "Mungu wangu, Mungu wangu mbona umeniacha?" (Mt 27:46). Mtegemee Mungu katika yote.


Msalaba ni tangazo la msamaha na huruma ya Mungu kwetu: Uwasamehe kwa kuwa hawajui watendalo. Toa msamaha kwa waliokukosea uwe mtu huru.


Msalaba ndiyo utimilifu wa kazi ya ukombozi wetu : "Yametimia." (Yn 19:30). Ishi upendo: utimilifu wa sheria. Ishi kwa ajili ya mafaa ya wengine kwa kujitoa sadaka kama Kristo naye alivyojitoa kwa ajili yetu.


"Ee Bwana tunakushukuru, tuakuabudu: Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako Mtakatifu"

Nakutakia tafakari njema.. 


Changia tafakari yako hapa

Post a Comment

0 Comments