Kuna mambo Mungu anakuruhusu Uyapitie ili uje kuwa Msaada Kwa wengine. Anakupa “Experience” muhimu ili uwe mwalimu mzuri kwa watu wengine hapo baadaye.
Masomo ya namna hii wakati mwingine yanaambatana na maumivu, kukataliwa na aibu ila ndio sehemu ya mtaala wa somo lako ili uandaliwe vizuri.
Sio kila unachopitia ni kwa ajili yako, kuna mengine yanakuandaa kuwa msaada kwa wengine.
Unapitia makosa ambayo ulidhani usingeweza kuyafanya ili ukikutana na mtu aliyekosea USIMUHUKUMU.
Unapitia maumivu yanayodhihirisha udhaifu wako, ili ukikutana na na mtu aliyepatwa na aibu UMSITIRI.
Unakutana na kufeli katika kitu ulichokuwa na uhakika 100% kuwa utafaulu ili ukikutana na aliyefeli usimuone mzembe bali UMTIE MOYO.
Unapitia hali ngumu ya maisha na kukosa pesa, ili siku mtu akihitaji msaada wako kidogo unakuwa unaelewa maumivu ya kushinda njaa na kutokuwa na pesa.
Unapitia kipindi unabaki peke yako na hakuna wa kukusaidia ili siku ukikutana na mtu aliyeachwa na awapendao uelewe maumivu anayopitia na UMSAIDIE.
Kuna mambo ni kama kusomea udaktari, unasoma mambo magumu kwa miaka mingi ili uwasaidie wengine watakapougua. Kuna masomo ya maisha unayapitia leo ili uwe mwalimu na msaada kwa wengine.
Nakuombea, Mungu akupe nguvu usikimbie darasa bali UFAULU.
0 Comments