NIMESUKUMWA NIKUPE POINTS 10 ZA KUKUSAIDIA KUISHI NA WATU #TAFAKARI


1. Ishi na watu wote,ongea na kila mtu... usimpapalikie mtu eti kwasababu ya cheo chake au kwasababu atakusaidia au alikusaidia kitu,kwasababu ya pesa zake.

2. Usimpuuze mtu kwasababu ya uhitaji  wake, uduni wake,au kwa kuyumba kwa dishi lake au kukatika kwa pistoni zake 

3. Usimchukie mtu eti kisa hakuja kukuona kwenye msiba,hakukuchangia kwenye send off,harusi,na tamasha, elewa tu haya maisha yako na changamoto nyingi sana....kimsingi hakuna mtu asiyependa kwenda msibani na kuhudhuria sherehe.

4. Usiwe wa kwanza kutengeneza chuki au bifu na mtu afadhari ukawa wa kwanza kutengeneza amani na mtu......

5. Usiwe chanzo cha kuleta makwazo....NA ukigundua umemkwaza mtu basi uwe mwepesi kuomba radhi....hii ni kwasababu msamaha hushusha hasira na ghadhabu ya mtu.

~Luka 17:1

Makwazo hayana budi kuja, lakini ole wake mtu yule ambaye yaja kwa sababu yake!

6. Ukijigundua kinywa chako kinawakosesha raha watu wengine kiasi ambacho wanakuogopa hata kukusogelea kwa kuogopa mdomo wako, usione sifa Basi ujue mdomo wako ndio adui yako nambari moja kuliko hata shetani na utakukosesha mbingu....Anza kujaza Neno la Mungu kwa wingi ndani yako ili utumie midomo yako kuwashuhudia watu injili waje kwa Yesu....na ujazwe roho uanze kunena na lugha.

Namaanisha hivi;

Ukiona kiungo chako kinakukosesha kinatumiwa na shetani ujue umebadiri matumizi.

7. Ukiona ulikosana na mtu hata kama yeye ndiye mkosa aliyekukosea na huyo mtu ukaona nyumba yake inaungua moto,hukwenda kumwokolea hata sufuria au ukaona ng'ombe wake anajisokota kamba kwenye kichaka karibu ajinyonge....kisha ukajisemea moyoni mwako, "kila mtu apambane na hali yake" 

Basi elewa huna moyo wa Mungu ndani yako, na wewe unaweza kuwa adui wa huyo mtu na si yeye kuwa adui yako.

8. Wakati mwingine ni vizuri sana kufanya kazi iliyopo kuliko kukaa na kusubiri kazi ya ndoto yako.....lakini chunga sana hiyo iliyopo isikuzoee au wewe kuizoea hadi ukaridhika nayo maana hiyo ni kazi ya mkate tu lkn si ya kukufanya utimize ndoto yako.

9. Nikupe mbinu bora ya kujibiwa maombi yako kwa haraka;

Kila unapoomba usiache kutoa sadaka ukiunganisha na maombi yako.

10. Moja ya mambo yanayochangia ndoa kuwa mizozo isiyokwisha, ni mke kutokusimama kwenye eneo lake la kubonyea kwa mume....kutokuwa mtii,pamoja na malumbano ya maneno.

Yaani wanaume hasa wanyakyu hatupendi dharau na majibizano ya kulumbana (Ulukwabho) sijajua kwa makabila mengine.

Yaani hakuna kitu kizuri kama unamwambia mke kitu hata kama umekasirika, anakusikilizaa halafu ukishamaliza anasema Nisamehe baba nakiri nimekosea na hakitajirudia.

Sasa ndugu zangu wadada wa kileo japo si wote, mwanaume unaongea,naye anaongea kama wimbo wa kolabo.....unamwambia Mimi ni kichwa hapa ndani! Naye anajibu "Namimi ni shingo sasa tuone kama kichwa kinakaa bila shingo!😏😏😏"  na akigundua amekosea anasema ee yameisha basi😐

WANAWAKE JIFUNZENI KWA MAMA ZENU AU BIBI ZENU WALIVYOISHI NA WAUME ZAOO NDIO SIRI YA NDOA ZAO KUDUMU HADI UZEENI!

Post a Comment

0 Comments