IMANI NI NINI?




IMANI NI NINI ?
 ✔Warumi 10:17 
“Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.”ll

Pia Imani unaweza Sema hivi,

BILA IMANI HUWEZI KUMPENDEZA MUNGU 
✔Waebrania 11 
Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.

MUNGU HAPENDI WANAOSITA SITA HATA KIDOGO 
✔Waebrania 10 
Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia.
Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye.
Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.


ISHI KWA IMANI YA MUNGU ACHA KUKATA TAMAA
 ✔Warumi 1:17 
“Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa imani.


USIFUATE MIKUMBO ISIYO NA IMANI THABITI
✔  1 Timotheo 1:19 
“uwe mwenye imani na dhamiri njema, ambayo wengine wameisukumia mbali, wakaangamia kwa habari ya Imani.

TIMIZA JUKUMU LAKO KWA WEMA
 ✔ 1 Timotheo 6:12 
“Piga vita vile vizuri vya imani; shika uzima ule wa milele ulioitiwa, ukaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi

OMBA KWA IMANI NA MUNGU ATAKUJIBU
✔Yakobo 5 
Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa.
 Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.

Nakutakia tafakari njema...

Andika comment yako hapa

Post a Comment

0 Comments