- Nyati wanaua watu 7 kila mwaka.
- Simba wanaua watu 500 kila mwaka.
- Kiboko wanaua watu 800 kila mwaka.
- Mabuibui wanaua watu 5000 kila mwaka.
- Nnge wanaua watu 7000 kila mwaka.
- Nyoka wanaua watu 10000 kila mwaka.
Kisa cha kushangaza,
Mbu wanaua watu milioni 2.7 kila mwaka...! Ndio... Walio wadogo kabisa ndio wanaoua sana..!!
Dhambi ndogo ndogo, ambazo wengi hawazioni au hawazitambui, ndio zenye kuua zaidi maisha yako ya kiroho (imani).
Epuka kutosali kutenga muda mchache wa siku yako kwa ajili ya Mungu wako.
Dhambi za upungufu zinaua kama dhambi za uamuzi tu..!
Kusengenya na uongo mdogo mdogo, kunafanywa mara kwa mara na ndio mauti.
Chunga yale madogo madogo unayoyafanya kila siku, ndio yatakayo kuangusha.
Watu wa kufanikiwa wana mambo mawili midomoni mwao: Tabasamu na Kimya
Tabasamu inaweza kutatua matatizo, na kimya kinaweza kuepusha matatizo.
Sukari inaweza kuchanganywa na chumvi, lakini siafu wanaikataa chumvi na wanaibeba sukari pekee.
Chagua watu wa sawa katika maisha, uyafanye maisha yako yawe bora na matamu.
Ukishindwa kufikia ndoto zako, badilisha mbinu wala sio Mungu wako
Kumbuka miti hubadilisha majani yake, wala sio mizizi yake.
Hutafikia unakokwenda (lengo lako) ikiwa utasimama kurushia mawe kila mbwa anaye kubwekea.
Wapinzani wakikuona unatembea kwenye maji, watasema ni kwasababu huwezi kuogelea.
Hata ukicheza kwenye maji, maadui wako watalalamika unarusha vumbi.
Fanya hamu yako iwe kuishi maisha ya utulivu, kutizama yako, na kufanya kazi kwa mikono yako.
Kumbuka usishindane hata na nguruwe... Mtachafuka nyote lakini nguruwe atafurahia..!
Kuwa mwenye hekima
Kosa mahali popote ila kwa Mungu usikose.
Tafadhali usidharau dhambi ndogo ndogo
utajutia kuikosa Mbingu
Yangu ni hayo tuu kwa siku ya leo, naamini umejifunza mengi kupitia Makala hii, endelea kufuatilia Makala zetu uzidi kujifunza mengi zaidi,
Ahsante na nakutakia siku njema.
0 Comments