UNGANA NAMI TUJADILI SUALA HILI 🤔🤔
"Yule Joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani AUDANGANYAYE ULIMWENGU WOTE..." (Ufunuo 12:9)
"Na Manabii WENGI wa uongo watatokea na KUDANGANYA WENGI."
(Mathayo 24:11)
"Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; Maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni WENGI waingiao kwa mlango huo"
(Mathayo 7:13)
"WENGI wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, sikuwajua ninyi kamwe, ondokeni kwangu ninyi mtendao maovu." (Mathayo 7:22,23)
"Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa Katika Kitabu cha mwanakondoo aliyechinjwa tangu Kuwekwa misingi ya Dunia."
(Ufunuo 13:8)
"Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ISHARA KUBWA na MAAJABU ; wapate kuwapoteza, kama yamkini hata walio wateule." (Mathayo 24: 24)
"Nikaona Roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule Joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. Hizi ndizo Roho za mashetani zifanyazo ishara..." (16:13,14)
JE!, WATU WOTE WATADANGANYWA?
Biblia inasema ni watu wachache wataokolewa!!!
"Bali mlango ni mwembamba na njia imesonga iendayo uzimani nao waionayo ni wachache" (Mathayo 7:14)
"Msiogope enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme." (Luka 12:32)
SILAHA ATUMIAZO SHETANI KUUDANGANYA ULIMWENGU.
1.SHETANI ANATUMIA WATU WAKE WAFANYE MIUJIZA NA ISHARA ZA UONGO ILI AWADANGANYE.
"Kwa maana watatokea makristo wa uongo na manabii wa uongo nao WATATOA ISHARA KUBWA na MAAJABU wapate KUWAPOTEZA yumkini hata walio WATEULE."
(Mathayo 24:24)
"Naye afanya ISHARA kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi, mbele ya Wanadamu. Naye AWAKOSESHA wale wakaao juu ya nchi kwa ISHARA zile alizopewa kuzifanya..."
(Ufunuo 13:13,14)
"Yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, NA ISHARA NA AJABU ZA UONGO; na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao WANAOPOTEA kwa sababu HAWAKUKUBALI KUIPENDA ILE KWELI WAPATE KUOKOLEWA."
(2 Wathesalonike 2: 9,10)
"Na Manabii wengi wa uongo watatokea na KUDANGANYA WENGI"
(Mathayo 24:11)
"Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao."
(2 Wakorintho 11: 14,15)
2:SHETANI ANATUMIA WATU WAKE NA SERIKALI KULAZIMISHA WATU WAFANYE IBADA ZA UONGO.
"Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye VITA juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao AMRI ZA MUNGU NA KUWA NA USHUHUDA WA YESU..."
(Ufunuo 12:17)
"...Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudu mnyama wa kwanza..."
(Ufunuo 13:12)
"Tena alipewa KUFANYA VITA na watakatifu na kuwashinda..."
(Ufunuo 13:7)
TUTAMSHINDAJE SHETANI?
1.Mpokee Yesu na Shika neno lake, uwe mwaminifu hata Kama ni kufa lakini usitende dhambi.
"Nao wakamshinda kwa damu ya mwana kondoo, na kwa neno la Ushuhuda wao, ambao hawakupenda maisha yao hata kufa"
(Ufunuo 12:11)
"...Uwe mwaminifu hata kufa Nami nitakupa taji ya uzima." (Ufunuo 2:10)
2.Shika amri kumi za Mungu.
Shetani anavita na washikao amri za Mungu. Usiwe upande wa wapinga amri za Mungu, upande huo ni wa Shetani. Fanya kinyume cha Shetani.
"Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu na kuwa na Ushuhuda wa Yesu..." (Ufunuo 12:17)
"Mkinipenda mtazishika amri zangu" (Yohana 14:15)
"Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu" (Ufunuo 14:12)
3.Usitishwe na miujiza, tii neno la Mungu.
"mtu ataishi kwa kila neno litokalo Katika kinywa cha Mungu."
(Mathayo 4:10)
Biblia inaikubali miujiza ya kweli.
Hata Manabii, mitume na Yesu walifanya miujiza.
(2 Wafalme 4:1- 5:19; Matendo 3:1-10; Matendo 20:7-12; Yohana11:1-44) Lakini hawakukataa amri za Mungu wala neno la Mungu na kujikita katika miujiza kama wafanyavyo mamilioni wa leo. "Uwatakase kwa ile kweli, neno lako ndiyo kweli" (Yohana 17:17)
Ulimwenguni wa leo umekataa amri za Mungu na neno lake na kukumbatia miujiza, hivyo Shetani anawatimizia haja zao za miujiza waitakayo.
Biblia inasema miujiza itaupoteza ulimwengu wote kama yamkini hata wateule watapotea. (Mathayo 24:24; 2 Wathesalonike 2:9-12; Ufunuo 13:13,14)
"Na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; Kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa. Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu wauamini uongo ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, Bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu."
(2 Wathesalonike 2:10-12)
5. Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu ibilisi, kama Simba angurumaye, huzunguka zunguka akitafuta mtu ammeze. (1Petro 5:8,9)
0 Comments