MWANAUME ELEWA KUWA MWANAMKE ANAPENDA KUSIKILIZWA


Bila kupoteza wakati.....nenda nayo......

Unaweza ukashangaa.. na usielewe... lakini ukweli ndio huo.. mwanamke anapokua na shida huwa anataka kusikilizwa kwa muda huo.. na wala sio kutatuliwa shida bila kutafakari ....
Angalia huu mfano hapa chini.. kati ya Lucy na Andrew... ambapo lucy amerudi nyumbani akiwa amechoka na ana matatizo lukuki kichwani mwake.. basi anaamua kushare na mpenzi wake Andrew..

maongezi yalikuwa kama hivi...

LUCY; "yaani kazi nyingii, mambo mengi mpaka nakosa muda wa kufanya mambo yangu."

ANDREW; "inabidi uache hiyo kazi, huhitaji kufanya kazi nyiingi.. tafuta kazi utakayoipenda"

LUCY: "lakini naipenda kazi yangu.. tatizo wanataka nifanye mambo yote kwa wakati mmoja."

ANDREW: "usiwe unawasikiliza.. wewe fanya unachoweza kufanya basi"

LUCY: "ooh my God ona sasa mpaka nimesahau kumpigia simu shangazi"

ANDREW: "usijali.. atakuelewa tuu"

LUCY: "hivi unajua ni wakati gani mgumu anaoupitia sasahivi? ananihitaji saana aargh"

ANDREW: "daah tatizo you are worrying too much ndio maana muda mwingi hauna furaha"

LUCY; "sio kwamba sina furaha.. hivi ni kwanini huwezi kunisikiliza??"

ANDREW: "aah.. hapana.. mbona nakusikiliza"

LUCY; "au naonekana msumbufu kwako si ndio??"

Baada ya hayo mazungumzo Lucy alipitiliza mpaka chumbani akiwa amejawa huzuni, hasira na kuhisi kuchanganyikiwa zaidi.. baada ya kuchanganywa huko kazini kwake na nyumbani pia.. mpenzi wake kamvuruga zaidi..

🤔🤔🤔
Unaona.. basi hali hii ndio ipo kwenye mahusiano mengi.... na tatizo hili limekuwa kubwa zaidi na kuhatarisha mahusiano mengi..

lakini umeishajiuliza mfano maongezi hayo yangeenda kama hivi hapa chini...

LUCY: "yaani kazi nyiingi.. mambo meengi mpaka nakosa muda wa kufanya mambo yangu,"

ANDREW: "pole saana baby.. inaonekana ulikuwa na siku nzito sana leo?"

LUCY; "yaani wanataka nifanye mambo mengi kwa wakati mmoja"

ANDREW: "hmmmhh.. pole baby.."

LUCY: "yaani mpaka nimesahau kumpigia simu shangazi yangu"

ANDREW: "ooh No.. sasa tutafanyeje?"

LUCY: " anapitia kipindi kigumu sana sasahivi ananihitaji saana"

ANDREW: "nafahamu baby.. una moyo wa kipekee sana mpenzi wangu.. njoo hapa nikukumbatie.."

Lucy akasogea kwa Andrew.. kisha andrew akamkumbatia kwa nguvu na kumfanya Lucy ajisikie vizuri saaana..

😊😊😊
eenhe.. unaona..?? hicho ndicho wanachohitaji Wanawake... wanahitaji kusikilizwa sio kutatuliwa matatizo..

lakini usinielewe vibaya eti kwamba hawahitaji kutatuliwa matatizo.. NO.. utatuzi unahitaji lakini sio kwa muda huo ambao anakuwa amechanganyikiwa.. na hajui chakufanya.. muda huo anakua nahitaji kusikilizwa saana... na badae kabisaa baada ya muda fulani akishatulia ndio utatuzi ufanyike...
😊😊

zingatia hayo sometimes huwa napenda kusema take it

Ili mke awe available kwa mume kimwili na kiroho
inampasa mume awe na sifa zifuatazo:
Ukaribu, uwazi katika mambo yake, anayeeleweka, mtu wa amani, anayempa uhakika mke kwamba ni yeye peke yake ndiye anapendwa na mume wake na pia kumpa uhakika kwamba yeye ni mwanamke mwenye sifa anazozipenda kimwili (beauty) na kiroho.

Je, unawezaje kuwa mume ambaye mke anakuelewa?
Ili mke akuelewe mume unahitaji kutumia secret weapon ya sikio lako.
Kumsikiliza tu mke huweza kuonesha kwake kwamba umemuelewa kuliko hata kabla hajamaliza kuongea wewe unamkatiza na kusema ulikuwa unajua anataka kusema kitu gani.

Tofauti kubwa ya mwanamke na mwanaume ni kwamba mwanaume kawaida yupo wired kusikilizwa na si kusikiliza, na mara nyingi mwanaume hupenda kutatua tatizo au matatizo au kutoa jibu kwa ajili ya tatizo lolote, hivyo anapoongea na mke wake kwa kutomfahamu anakuwa na haraka ya kutaka kutoa majibu badala ya kusikiliza tu.
Narudia tena!!;
Si mara zote mwanamke anapouliza swali au kukwambia kitu anahitaji majibu, mara nyingi anakuwa katika harakati ya kujikusanisha (connection) na wewe na anachohitaji ni sikio lako tu na si namna ya kupata majibu.

Unachotakiwa kufanya ni kumsikiliza na kushiriki katika kuzungumzia hiyo shida yake na kuliona kama tatizo lenu wote.
Mwanamke huhitaji mtu wa kumsikiliza tu na sikio lako wewe mume ndilo analihitaji na si uwezo wako wa kutatua tatizo.

Ukimsikiliza, atajisikia vizuri tofauti na ukirukia kukatiza kile anachoongea au kuanza kupendekeza solutions kwa kile anachokwambia.

Wanaume kujitahidi kutoa solutions za kile mke anachooongea au hata kukatiza kile anachoongea kwa mume kujifanya anajua mke alitaka kuongea kitu gani ni moja ya matatizo sugu ya kwenye ndoa.
Hata kama wewe ni mwanaume maarufu kutatua matatizo ya wanaume wenzako bado ukiwa na mke wako unatakiwa kumsikiliza tu na sikio lako hadi aridhike.

Nawapenda sana...!!!!

Post a Comment

0 Comments