FAHAMU KUHUSU UTOSI WA MTOTO NA LINI UNAFUNGA.



Mojawapo ya sehemu zinazohitaji uangalizi wa hali ya juu katika mwili wa mtoto ni utosi.
Kitaalamu utosi unaitwa Fontanelle neno liliotokana na lugha ya kilatini (Fonticulus) ikimaanisha kitu kama spring.Uwepo wa utosi ni muhimu kwa kuwezesha ubongo kukua na kuongezeka size yake.

UTOSI NI NINI?
Kikawaida fuvu la kichwa la mtoto linakuwa limeundwa na muunganiko wa mifupa 6 ambayo imeunganishwa na tishu zinazovutika na laini zinazojulikana kitaalamu kama sutures.
Tishu hizi (sutures) zinakua zimejishikiza na kuunganisha mifupa yote sita ya fuvu la kichwa.Katikati ya mfupa mmoja na mwingine palipo na hii tishu(suture) ndipo panaitwa utosi.


Zipo aina sita za utosi, japokuwa kubwa ni mbili.Aina mbili kubwa za utosi ni Utosi wa mbele (anterior fontanelle) na utosi wa nyuma(posterior fontanelle) aina ambayo huonekana sana ni huo utosi wa mbeli ambao huchelewa kufunga.
Utosi wa mbele unakuwa katikati ya mfupa wa mbele (Frontal bone) na mifupa ya pembeni (parietal bones) na utosi wa nyuma unakua kati ya mfupa wa nyuma au kisogo na mifupa ya pembeni ya kichwa kama mchoro huu unavoonyesha
Aina nyingine za utosi ndogo ni sphenoid fontanelles na astoid fontanelles ambazo zinakua katikati ya mifupa ya pembeni ya kichwa


JE UTOSI HUFUNGA BAADA YA MUDA GANI?

Utosi wa mbele ndio huchelewa kufunga, ambapo huchukua muda kati ya miezi 18 hadi 24 kufunga.Utosi wa nyuma wenyewe hufunga ndani ya muda wa miezi mitatu(3).
Aina zile nyingine za utosi za pembeni hufunga baada ya mwezi mmoja tokea mtoto azaliwe,na kutokana na kuwa ndogo sana sio rahisi kuziona.

VITU VYA KUZINGATIA WAKATI UTOSI HAUJAFUNGA
Kutokana na tishu za katikati ya utosi kuwa bado laini inaweza kupelekea kichwa cha mtoto kubonyea na kubadili umbo la kichwa kutokana na mgandamizo kwenye kichwa,mgandamizo unaweza kutokana na jinsi unavyomlaza mtoto wako.kichwa kinaweza kuwa flat sehemu iliyogandamizwa hali hii kitaalamu inaitwa  brachycephaly.

Ni muhimu kuzingatia jinsi gani unamlza mtoto ili kuepuka kupata shida hii. Inashauliwa mtoto alalie mgongo hii itamuepusha na tatizo hilo.

KARIBUNI SANA

Post a Comment

0 Comments