FUNGUO SAHIHI KWA KUFULI SAHIHI


Hivi umewahi kujiuliza kwanini kituo huwekwa mwishoni mwa neno na si alama ya Koma?? Au umewahi kujiuliza kwanini mabasi hufikia kituo cha mabasi na si nyumbani kwa dereva?? Au umewahi kujiuliza kwanini makufuli hufunguliwa kwa funguo zake sahihi na si zingine?? Hizo ni terminologies ambazo wengi huwa hawajui maana zake.

Ni vyema mwanamke au mwanaume kuweka kituo kikuu kwenye uchaguzi wake wa mahusiano na si vinginevyo. Yamkini umekutana na funguo nyingi zisizoweza fungua kufuli lako na kila ulipojaribisha ziligoma lakini leo umebahatika kupata funguo sahihi basi nakusihi leo tunza funguo wako wala usiruhusu kujaribisha kufungua kufuli lingine lisilofaa.

Jaribu kushuka kwenye kituo uendacho na si kujaribu kishuka kwenye kituo ambacho si chako unaweza kupotea kabisaa, tena usijaribu kuweka koma mwishoni mwa neno maana itakufanya kuendelea kuandika maneno mengine yasiyofaa kwako weka kituo ili uwe na mwisho mzuri wa neno lako.

Always tabasamu kwa kumpata uliyemtafuta miaka mingi na leo umempata unaweza kuwa umekutana na mamia ya watu lakini leo umefunga break kwa mtu mmoja tuu kama maandiko yasemavyo. Basi jaribu kuimarisha break zako zisiachie tena mpende na umfanye awe wako, usijaribu kumfananisha na mamia yaliyopita maana yeye ni mwanzo mpya na mwisho mzuri kwako....

Post a Comment

0 Comments