𝐃𝐡𝐚𝐫𝐚𝐮 Z𝐚𝐤𝐨 Z𝐢𝐭𝐚𝐤𝐮𝐩𝐨𝐧𝐳𝐚 S𝐢𝐤𝐮 M𝐨𝐣𝐚,



Hebu Jifunze kumuheshimu kila mmoja pasipo Kujali umri au Cheo alichonacho kwasababu Unaweza ukahisi umefanikiwa Sana kwenye maisha yako lakini Kumbe bado mno nakwambia hivyo  kwasababu hauwezi kufanikiwa katika kila kitu,

𝐌𝐚𝐟𝐚𝐧𝐢𝐤𝐢𝐨 𝐲𝐚 mtu huwa yanapimwa kwa namna kuu nne (4) Moja wapo ni Imani,Mbili ni Fedha (Mali),Tatu ni Elimu (Taaluma) na mwisho kabisa ni Umaarufu (Kujulikana).

Sasa ajabu ni kwamba Unaweza Ukawa na pesa lakini usiwe na Imani ,Unaweza Ukawa maarufu lakini usiwe na pesa Au ukawa na Elimu kuuubwa lakini usiwe na Pesa ya kutosha kwahiyo Usipotoshwe na Fedha ukidhani ndiyo kipimo pekee Cha mafanikio ya mtu kwasababu kuwa na Afya njema pia  nayo ni mafanikio tosha.

Sikiliza nikwambie hata wewe una kila sababu ya kufanikiwa kwenye maisha yako Tena sana tu Sema Tatizo unajidharau na umejisahau Sana.

Hakuna Shaka Tena juu ya Nini MTU anapaswa Kufanya ili afanikiwe  kwani Siri imefichuka (Mambo yapo wazi).

𝐇𝐚𝐲𝐚 𝐧𝐝𝐢𝐲𝐨 𝐌𝐚𝐦𝐛𝐨 𝐤𝐮𝐮 9 𝐚𝐦𝐛𝐚𝐲𝐨 𝐮𝐧𝐚𝐩𝐚𝐬𝐰𝐚 𝐤𝐮𝐲𝐚𝐟𝐚𝐧𝐲𝐚 𝐢𝐥𝐢 𝐮𝐟𝐚𝐧𝐢𝐤𝐢𝐰𝐞 𝐤𝐰𝐚 𝐯𝐢𝐰𝐚𝐧𝐠𝐨 𝐯𝐢𝐤𝐮𝐛𝐰a.

1. Lifahamu Kusudi lako.
2. Chagua Jambo Moja (Niche)
3. Tafuta Maarifa/Knowledge.
4. Tafuta Msimamizi/Mentor.
5. Weka Malengo/Lengo.
6. Gharamia malengo yako
7. Tekeleza kwa dhati.
8. Vumilia na Subiria.
9. Fanikiwa zaidi.


Ukifanya Mambo hayo 9 kwa uaminifu kabisa Basi ni wazi mafanikio yatakuwa sehemu ya Maisha yako na Utashangaa. Swali ni je Wewe unataka kufanikiwa katika Nini ? Na lini unataka uwe umefanikiwa ?

𝐇𝐚𝐭𝐚 𝐰𝐞𝐰𝐞 𝐔𝐧𝐚𝐰𝐞𝐳𝐚 𝐤𝐮𝐟𝐚𝐧𝐢𝐤𝐢𝐰𝐚 𝐉𝐢𝐚𝐦𝐢𝐧𝐢. 

Bila shaka unaweza ukawa bado Upo njia panda (Dilemma) hujui Nini ufanye na una Hofu (WOGA) umri unazidi kusogea na hujafanya chochote na pengine bado unaishi kwa watu au umeishi nyumba za kupanga kwa muda mrefu na hujajenga hata kijijini kwenu,huna biashara yoyote Ila Una pesa ya kutumia (Starehe) au Unaamka asubuhi ili ulale usiku na pengine Upo upo tu hujielewi kabisa unashinda ukiangalia series au Movie kila siku.



Usiogope kila kitu kitakuwa sawa.

Kwani bado hujachelewa kuamua.

Post a Comment

0 Comments