MWENYE SURA MBILI (MNAFIKI)

Huyu ni mtu ambae huenda akawa ni ndugu au rafiki yako wa karibu zaidi, bila kujua unamuamini unampa siri zako na malengo yako ya kimaisha ukitaraji kuwa ni msaidizi wqko katika maisha, 

Ghafla ukaja kujua au kuona mambo yako hayaendi wala hufanikiwi huku ukijiuliza sababu ni nini? Unakuja kugundua kumbe huyo unayempa siri zako au anaona mafanikio yako au bidii yako ndo adui yako, 

Unabaki unashangaa tu wala huamini, mtu ambae alikuwa anakupa maneno mazuri bin matamu, au anaonyesha kuwa mstari wa mbele katika kukusaidia kila upatapo na shida kumbe ndo yupo mstari wa mbele katika kukuangamiza,

Usipaniki wala kukasirika baada ya kumgundua, bali jiweke mbali nae huku ukimuombea maisha marefu ili aone mafanikio yako, Mungu amewaahidi adhabu kali watu wa aina hii, wenye kufitinisha watu na kuwafanyia uhasidi wenzao,

Ewe mwenye tabia hii acha haraka kwani kila ufanyalo litakurudia mwenyewe na utalipwa kwa kila ufanyalo,

Post a Comment

0 Comments