NENO LA MUNGU LINANGUVU KULIKO LA MWANADAMU

Anza Siku na Bwana, maliza Siku na Bwana, 
Mshirikishe Mungu katika kila jambo,

Karibuni leo tutafakari Nemo hili ambalo litakufanya utambue kuwa matendo ya mungu ni makuu kuliko ya binadamu, kwa namna nyingine twaweza sema Neno la Mungu ni Kuu kuliko la binadamu yeyote, 

Karibu, endelea nayo.....

 ZABURI 37:25&26
Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzao wake akiomba chakula.
Mchana kutwa hufadhili na kukopesha, Na mzao wake hubarikiwa.

  Mpendwa jifunze;
  • Mungu hamwachi mtu mwenye haki. 
  • Mungu ndiye mfadhili wa mwenye haki.  
 Mpendwa,
1.Je, wewe umewahi kuona mwenye haki ameachwa na Mungu?
2.Je, wewe umewahi kuona mzao wake ukiomba chakula?

  TAFAKARI
    Mpendwa, Mungu ndiye Mfadhili wa wenye HAKI. Mwenye haki ni mtu ambaye anamcha Mungu na kujiepusha na UOVU . Kinyume cha haki ni uovu na kinyume cha mwenye haki ni mwovu yaani mwenye dhambi 
  •  Mwenye haki ni mtu aliyetubu na anayekwenda kwa ukamilifu na kwa unyenyekevu mbele za Mungu. Moyo wake hupendezwa na njia za Mungu.
  • Mtu anaye hesabiwa kuwa ni mwenye haki, ni yule anayeshika na kulifuata neno la Mungu, na sheria za Mungu ambayo ni maagizo yake yote atupatiayo kupitia neno lake. EZEKIELI 18:9 "tena ikiwa amezifuata sheria zangu, na kuzishika hukumu zangu; mtu huyu ni mwenye haki; hakika ataishi, asema Bwana MUNGU.”
  • Mwenye haki ana ujasiri wa kusimama mbele za Mungu na ana hakika kwamba muda wowote akifa anaingia mbinguni lakini mwovu hana ujasiri wa kusimama mbele za Mungu wala hawezi kuufurahia uwepo wa Mungu kwasababu yeye ni mchafu na badala yake hataki kabisa kusikia habari za YESU KRISTO kwasababu anagusa maisha yake na kumfanya akose amani.
  • Mwenye haki anapenda amani , na kwa kupenda amani anakuwa anampenda Yesu aliye mfalme wa amani.
Kumbuka, Mungu atawatenga wenye haki na waovu siku ile ya hukumu.
 Je, wewe utakuwa upande upi?
    MATHAYO 13:43
 Ndipo wenye haki no watakapong'aa kama jua katika ufalme wa Baba yao. Mwenye masikio, na asikie.

Barikiwa sana mtu wa Mungu.
 
Uwe na siku njema sana....


Andika comment yako hapa

Post a Comment

0 Comments