- Madhumuni ya muziki,
- mtindo wa muziki, na
- maudhui ya maneno ya wimbo.
Kwa hiyo unapoimba 'sisi tu maskini' unakuwa unautengeneza umasikini katika ulimwengu wa kiroho na si muda umasikini huo utakuja kujitokeza katika masha ya kimwili.
Mtu yeyote aliye hai kiroho hawezi kukiri au kusema sema hovyo hovyo kwa kuwa kwa kusema sema hovyo huko ndio kunapelekea hayo mambo kutokea katika maisha yake.
Mfano:Kukiri “kushindwa”nawe utashindwa ,ukikiri “maisha magumu” na kweli kwako wewe yatakuwa maisha magumu hata kama yalitaka kuwa maraisi kwa kuwa shetani atashikilia uthibitisho wa neno lako ulilolisema.
Kwa hiyo kutokana na muziki wa dunia utajikuta kwenye hatari ya kujikuta ukiimba vitu visivyo na maana ukadhani inaishia hapo tuu,kumbe inakwenda kuathiri ulimwengu wako wa kiroho kwa kukiri vibaya baadhi ya mambo katika maisha yako tuu kwa sababu ya kufuatisha na kuziimba nyimbo za kidunia.
Kupitia muundo wa video za miziki ya kidunia kuna baadhi ya vitendo vyao katika mkanda(scene) vinakuunganisha na ushetani.
Hivyo kwa kusikiliza miziki ya kidunia unaweza jikuta ukipatanishwa na kuzimu kutokana na maagano husika juu ya miziki yao.
Kuingia na tamaa
Imeandikwa “Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;” Wakolosai 3:5
Video nyingi za muziki wa kidunia huwa na namna ambayo huamsha watu wanao zitazama hali ya kutamani wanawake,pombe na ngono.Video hizo ambazo wasanii huvaa nusu uchi na kucheza kwa kuonyesha maungo yao ili tuu kutamanisha.
Mungu hapendi sisi kama wanawe tuingie katika tamaa zozote bali hupenda tuzishike sheria zake na tuzifuate. “Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.” 2Timotheo 2:22
Hivyo basi kwa kuziangalia video za muziki wa kidunia mara nyingi unaweza kujikuta ukiingia katika tamaa na kwa hiyo tamaa unakuwa umemkosea MUNGU na unapokuwa umemkosea MUNGU hapo ndipo ulinzi wa Mungu huondoka maishani mwako na shetani kupata nafasi katika maisha yako.
Kwa hiyo ni bora kujiepusha kusikiliza na kufuatilia muziki wa kidunia kwa kuwa unakufanya uwe na tamaa ambazo mwishowe utaangamia kwa kuwa imeandikwa. Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.1 Yohana2:17
Kuweka hazina sana kwenye ngono,wanaume,wanawake kuliko MUNGU.
Imeandikwa “kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.” Mathayo 6:21
Badala ya kuweka hazina katika kujitoa katika kazi za MUNGU kwa fedha au hata nguvu basi kwa wanaosikiliza sana muziki wa kidunia hujikuta wakiweka hazina zao kwa wanawake,ngono mdawa ya kulevya.
Hili ni gonjwa la kiroho linalotokana na kusikiliza muziki wa kidunia.
Muziki wa kidunia una athari nyingi nazo hutengenezwa kidogo kidogo kama vile ulikuwa hujui kunywa pombe unaanza kunywa kidogo kidogo,
Ulikuwa huna tamaa za wanawake sasa waweza jikuta kutokana na video za muziki wa kidunia unaanza hamasika na kuwa na tamaa na wanawake.
1 Samweli 16:23
Ikawa, ile roho mbaya kutoka kwa Mungu ilipomjilia Sauli, ndipo Daudi akakishika kinubi, akakipiga kwa mkono wake, naye Sauli akaburudishwa, na ile roho mbaya ikamwacha.
Kila Muziki unaousikia masikioni mwako una nguvu nyuma yake na unazalisha aina ya Hisia ambazo au zitakusukuma ufanye jambo jema au ufanye dhambi.
Kila Muziki unasukumwa na tabia na roho inayofanya kazi kwa aliyeimba na waliopiga.
Muziki sio kitu cha kawaida kusema nasikia tu Bongoflavor kwani ni dhambi! ( Shida sio kwamba kusikia muziki wa Bongoflavor ni dhambi, bali kutakufanya uwe mshiriki muda si mrefu, muziki una nguvu)
TUANGALIE UPANDE WA SAULI NA DAUDI
Sauli anaingiwa na Pepo na linaanza kumsumbua na kumtesa
Daudi mwenye upako anapiga kinubi kwa ustadi na ghafla ile roho mbaya ndani ya Sauli inatoweka na Sauli anakuwa huru.
Maana yake kuna aina ya Muziki na upigaji ukiambatana na Roho inayofanya kazi kwa mwimbaji au mpigaji unaweza kutoa Pepo ndani ya Mtu na akawa huru
Vivyo hivyo kuna aina ya muziki na upigaji ambao unaweza kuingiza pepo ndani ya Mtu.
USICHUKULIE MUZIKI KAMA SEHEMU YA FURAHA
Elewa unaweza kuingiwa na mapepo kwa kuangalia Muziki.
Nitarudia Tena;
Muziki ni nguvu inayoweza kuharibu maisha ya mtu na hisia zake na kusababisha tamaa na mwisho dhambi na uharibifu.
Kwa mfano;
Unasikia Muziki wa Bongoflavor
Anayeimba anacheza na wadada wako Uchi na anawashikashika na biti na upigaji lazima uendane na step za kucheza na hisia za mwimbaji (Nakuhakikishia kuna roho za giza zinaingia kwenye maisha yako )
USICHUKULIE KUSIKILIZA MIZIKI YA BONGOFLAVOR KAMA KITU CHA KAWAIDA
wewe angalia mpaka hapo kama hisia zako na maisha yako yana usalama .
Angalia kwa umakini,
“ Usisikie kila wimbo na kila muziki, angalia miziki yenye nguvu za Mungu za kuponya Hisia zako na maisha yako ”
Isaya 55:3
Tegeni masikio yenu, na kunijia; Sikieni, na nafsi zenu zitaishi;
Kuna uzima kwenye kusikia
Lakini pia kuna kifo kwenye kusikia.
Kama una nyimbo nyingi za kidunia na chache za kumsifu MUNGU basi wewe tambua maisha yako ya kiroho yako kwenye hatari.
Chukua hatua na maisha yako yatakuwa salama,
0 Comments