1.0 UTANGULIZI
Zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Tano katika
Shule za Sekondari za Serikali, Vyuo vya Ualimu, na Vyuo vya Elimu ya
Ufundi kwa mwaka 2020, limefanyika na kukamilika. Zoezi hili
limefanyika kwa kuzingatia takwimu za matokeo ya watahiniwa
waliofanya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2019 kutoka Tanzania
Bara, idadi ya nafasi za Kidato cha Tano, Vyuo vya Ualimu, Vyuo vya
Elimu ya Ufundi pamoja na Vigezo vya Uchaguzi wa Wanafunzi
vilivyotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
1.1. TAKWIMU ZA WATAHINIWA WA MTIHANI WA KIDATO
CHA NNE, 2019
Watahiniwa wa shule 425,072 wakiwemo wasichana 221,813 na
wavulana 203,259 walifanya mtihani wa kuhitimu Kidato cha Nne
mwaka, 2019. Aidha, Watahiniwa wa Kujitegemea 48,683 walifanya
Mtihani huo mwaka, 2019.
Jumla ya wanafunzi 121,251 wakiwemo wasichana 53,829 na
wavulana 67,422 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano, Vyuo
vya Ualimu, na Vyuo vya Elimu ya Ufundi vinavyosimamiwa na Baraza
la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE). Idadi hii ni sawa na asilimia 93.4
ya wanafunzi wenye sifa za kuchaguliwa.
2. UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KUJIUNGA NA KIDATO
CHA TANO, VYUO VYA UALIMU NA VYUO VYA ELIMU YA
UFUNDI,
Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2020 ni
wale waliotoka Shule za Serikali, zisizo za Serikali, waliosoma nje ya
mfumo rasmi na waliosoma nje ya nchi baada ya matokeo yao kupata ulinganifu wa Baraza la Mtihani Tanzania. Jumla ya shule za sekondari
434 zikiwemo shule 32 mpya za Kidato cha Tano zilizoanza mwaka huu
zimepangiwa wanafunzi.
MAELEKEZO KWA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA
3.1 Wanafunzi wa Kidato cha Tano:
Wanafunzi wote wa bweni waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha
Tano mwaka, 2020 wanatakiwa kuripoti shuleni tarehe 18 Julai,5
2020 tayari kwa kuanza masomo tarehe 20 Julai 2020. Aidha,
wanafunzi wa kutwa waripoti na kuanza masomo tarehe 20 Julai
2020. Wanafunzi ambao hawataripoti wiki mbili tangu tarehe ya
kufungua shule nafasi zao zitachukuliwa na wanafunzi wengine
ambao hawakupangiwa shule katika awamu hii.
Uhamisho wa shule utaruhusiwa baada ya kukamilika kwa
Muhula wa Kwanza wa masomo, na zoezi hilo litafanyika kwa
kuzingatia uwepo wa nafasi kwenye Shule kwa idhini ya Maafisa
Elimu wa Mikoa husika. Hivyo, hakutakuwa na fursa ya kufanya
mabadiliko yoyote ya Shule kwa sasa ngazi za Mikoa
Halmashauri na shule.
3.2 Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Ufundi:
Wanafunzi waliopangwa kwenye Vyuo vya Elimu ya Ufundi
vilivyopo chini ya NACTE wanatakiwa:
i. Kuthibitisha kukubali kujiunga na kozi zinazosimamiwa na
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) baada ya siku
saba (7) kuanzia siku ya kutangazwa kwa matokeo ya
uchaguzi hadi tarehe 15 Agosti, 2020.
ii. Mwanafunzi atafanya uthibitisho kupitia kiunganishi
kinachoitwa Uthibitisho TAMISEMI katika tovuti ya Baraza
la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ambayo ni
www.nacte.go.tz ili kukubali kuchaguliwa kwenye kozi na
vyuo walivyopangiwa.
iii. Mwanafunzi ambaye hatathibitisha kukubali nafasi
aliyochaguliwa, nafasi yake itachukuliwa na wanafunzi
wengine wanaoendelea kuomba katika Vyuo hivyo kwa njia
ya mtandao.
0 Comments