WEKA BIDII YA KUMJUA MUNGU ILI UPATE NGUVU ZAKE.


Katika maisha ya hapa Duniani tumezungukwa na maadui Wengi sana kama somo la jana lilivyoelezewa. Ukimjua Mungu utapata silaha ambazo zitakusaidia kumshinda adui pamoja na kuweza kujiepusha na mambo mbalimbali ya Dunia him. Lakini    kuna faida nyingi sana unapomjua Mungu kama Ayubu anavyoeleza hapa chini :👇

 Ayubu 22:21
Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia.
**********************

Unapokuwa na nafasi ya kumkaribisha BWANA ndani yako unakuwa na amani na mema YATAKUJIA sio uyafuate maana Mungu mwenyewe atayaelekeza kwako kwa kuwatuma watu wengine wakuletee. 
Lakini wapo watu hawana muda na Mungu,  wanafanya mambo yao muda wote lakini nao wanazitazamia baraka za Bwana pamoja na nguvu zake. 

Unachotakowa katika utumishi ni kuwa na nguvu za Mungu ili iwe rahisi kukabiliana na mambo ya Dunia hii ni pamoja na kuweza kuvunja ngome za adui, na kuizima mishale ya mwovu Shetani. Mungu anasema tuzitake nguvu zake maana amejua kabisa bila ya kuwa na nguvu zake hatutaweza jambo lolote. Soma hapa👇

 Zaburi 105:4
Mtakeni Bwana na nguvu zake, Utafuteni uso wake sikuzote.
*********************

Kila mtu anatakiwa kufanya bidii katika kumtafuta Mungu ili aweze kupata nguvu, amani na mafanikio katika maisha yake.  Lakini wapo watu wanakula raha ya Dunia na wanasahau Kumtafuta Mungu na hatimaye wanakosa mambo mema zikiwemo nguvu za Mungu. Tuone mfano Wa watu ambao walikuwa wanajilisha upepo huku wakitaka kufanya ishara na miujiza kama wengine ambao wanatia bidii kumtafuta Mungu. 

 Matendo ya Mitume 19:13

Baadhi ya Wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo.
*********************

Hebu waone hao walivyoaibika,  Wanatumia Jina la Yesu wa Paulo wakati wao wanajilisha upepo,  wanakula raha, wanajirusha,  wanafanya kila aina ya mambo ya dunia kufurahisha mioyo yao lakini NDANI YAO HAKUNA NGUVU za Mungu, na hatimaye Mapepo yakawatolea uvivu🤔.

Nikuombe, fanya bidii umtafute Mungu nawe, utabarikiwa katika mambo yote. 
Yesu anasema yeye ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe,  hivyo mtafute Bwana nae atakuwa ndani yako, na utafanikiwa katika kila jambo.  Acha kujilisha upepo kwa mambo mengi ya Dunia hii. 

Mungu akubariki na kukupa neema ya kuwa na nguvu zake. Amina. 

Uwe na siku njema. 🙏


Post a Comment

0 Comments