Usipende kusoma, penda kujifunza kwa kile unachokisoma.

Usipende kuangalia movie, penda kujifunza kwa kile unachokiangalia.

Usiogope kukosea, penda kujifunza kwa kile unachokosea.

Usiogope kufanya, penda kujifunza kwa kile unachofanya.

Maisha ndivyo yalivyo, safari ya kujifunza haina mwisho. Jifunze kwa kila kitu kinachokuja maishani mwako, usiruhusu muda wako upotee bure. Jifunze kwa uzuri na hata kitu kikiwa kibaya tafuta kitu cha kujifunza kutokana na ubaya huo.

Ukikosea jifunze, ukifanikiwa jifunze. Ukishindwa uliza, utakuwa mjinga kwa dakika chache ukishaelekezwa utajifunza na utaelewa. Kamwe usiogope kuonekea hujui, hakuna aliyezaliwa anajua ila wote tumejifunza na kujua.

Jitahidi kila siku uwe unajifunza angalau kitu kimoja kwa kile unachokipenda. Mdogo mdogo na baada ya mwaka utajikuta umekuwa professional kabisa. Hiyo ndio nguvu ya kujifunza.

Hata mimi na najua vingi ila napenda kujifunza, msiniulize najifunza nini na nachukua siku ngapi kuelewa. hio ni siri yangu 😂.

Post a Comment

0 Comments