Upweke sio matokeo ya kutokuwa na mtu ila ni suala la kuwa na mtu ambaye hajui unataka nini au afanye nini ili upate furaha na msisimko halisi

Upweke sio matokeo ya kutokuwa na mtu ila ni suala la kuwa na mtu ambaye hajui unataka nini au afanye nini ili upate furaha na msisimko halisi.

Wapo wenye wapenzi ila bado ni wapweke kuliko wale walio single, matendo na tabia yako kwake ndio yenye kuamua ajihisi mpweke au awe na furaha.

Ikiwa hujui nini anapenda na unatakiwa kufanya nini na kwa wakati gani, kuna hatari ya mwenzako kujihisi mpweke angali yu-mikono mwako.

Kuwa naye muda wote ama kumpigia simu mara nyingi bila kumfanyia anayopenda ama atakayopenda sio sababu ya yeye kutojihisi mpweke, upweke ni matokeo ya yeye kutohisi furaha na msisimko wa kweli bila kujali amezungukwa na nini ama na nani.

Hata ukiwa katika kundi la watu lenye kupiga stori zinazowahusu wao tu ama wenye kujadili mambo usiyoyapenda ama kuyaelewa ni lazima utajihisi upweke, hivyo basi njia ya mwenzako kutokuwa mpweke sio tu wewe kuwa karibu yake ila kumtendea yenye kustahili na yalio na thamani kwake.


Post a Comment

0 Comments