SIMULIZI FUPI YENYE FUNZO KUBWA



Siku moja jamaa mmoja alichinja ng'ombe mnono na akachoma vizuri, baadaye akamwambia mke wake: "NENDA NA KAWAALIKE MARAFIKI NA MAJIRANI ZETU WAJE TULE NYAMA."


Basi mke mtu akatoka nje na kuanza kupiga kelele: "OH JAMANI MOTOO, TUNAOMBA MSAADA! MSAADA !! MOTOOO NYUMBANI KWETU !!!"

Kweli ghafla watu walitoka majumbani kwao lakini wengine walijifanya hawasikii chochote.

Basi wale walioingia ndani ya fensi ya nyumba hiyo walijikuta mbele ya "ndafu kubwa" ambapo walikula na kunywa hadi wakasaza.

Lakini baadaye yule jamaa alimgeukia mke wake, akamwuliza: "LAKINI MKE WANGU MBONA WALE ULIOWAALIKA SIWAJUI HATA MMOJA, WENGINE HATA SIJAWAHI KUWAONA. WAKO WAPI MARAFIKI NA MAJIRANI ZETU NILIKUAMBIA UWAAALIKE?"

Mke wake alijibu: "HAWA NDIO MAJIRANI NA MARAFIKI ZETU, WALE WALIOTOKA NYUMBANI KWAO KUTUOKOA SISI NA NYUMBA YETU. WANASTAHILI HESHIMA HII KWA SABABU HAWAKUTARAJIA KUPATA CHOCHOTE KWETU."

📌 UMEJIFUNZA NINI hapo?

#Imenikumbusha Luka 10:29

"Naye akitaka kujidai haki, alimwuliza Yesu, Na jirani yangu ni nani?"

#Jiulize: Who is your neighbor/friend? 📌

#YESUkwetuNiRafiki,

Somo    
Tusitende kwa kutegemea malipo tuzo Duniani kwani kwa Mungu hatuna cha kupoteza Mungu wetu ni Mungu Mwaminifu🙏🏻🙏🏻🙏🏻

Post a Comment

0 Comments