HIZI NI SIRI CHACHE ZITAKUSAIDIA KATIKA MAISHA YAKO HAPA DUNIANI

1. Kamwe usimchukie yule ambaye hakukusaidia ulipohitaji msaada wake au hakufanya vile ulitegemea angekufanyia. Hapana, usimchukie.

2. Kamwe usiache kumwomba Mungu au usiache kumuabudu hata kama hajajibu maombi yako, au amejibu Tofauti na ulivyoomba. Kumbuka Mungu si mwanadamu, yeye ni Mungu na hutuwazia mema.

3. Kamwe usijaribu wala usipange kulipiza kisasi kwa yule aliyekuumiza. Usipange hivyo wala usijaribu kufanya hayo. Hata kama alikuumiza mno, Usilipize kisasi.

4. Kamwe usiache kutenda yaliyo mema. Hata kama huoni anayekusifia, hata kama huni anayekuunga mkono, hata kama huoni anayekusaidia katika hilo, endelea kufanya yaliyo mema na sahihi, Mungu hatakuacha. Neno linasema, Wala tusichoke kutenda mema, kwani tutalipwa kwa wakati wake. Usipoona anayekuwa pamoja nawe au kukutia moyo, wewe endelea tu.

Wagalatia 6:9 Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho.

5. Katika maisha yako unaweza ukawa na maombi mengi juu ya maisha yako. Lakini ngoja nikupe siri, muda mwingine jifunze kuwaombea wengine pia. Mungu anapenda mtu anayewajali wengine. Kujiombea wewe tu ni ubinafsi. Hii siri jaribu kuifanyia kazi utakuja kuniambia.

Uwe na siku njema yenye baraka🤲🏻🤲🏻

Post a Comment

0 Comments