CHANGAMOTO YA KUFIKIA MALENGO, "BADO NAJIPANGA"😔



Moja ya CHANGAMOTO inayowachelewesha watu wengi sana kufikia malengo yao ni kila siku kuendelea "KUJIPANGA".

Yaani kuna watu miaka 10 sasa bado ukiwauliza mbona hawatekelezi mipango yao utasikia "BADO NAJIPANGA".

Kuna watu tangu mwaka umeanza hadi sasa hakuna walichofanya ukiwauliza watakuambia "BADO NAJIPANGA".

Kumbuka watu wa "Bado Najipanga" ndio wale ambao waliogopa kuanza kuishi ndoto zao na leo wameshazeeka.

Wanaopenda kusema bado najipanga ndio walewale waliosema ngoja nijishikize kidogo kwenye kazi hii nikisubiria ninayoitaka, na leo wameshatimiza miaka 10 hapo.

Ambao huu ni msemo wao, ndio wale ambao wenzao walishachukua hatua kubwa kusonga mbele na wamefika mbali....
...na wao ni kama wamekubali kuwa hawatafanikiwa zaidi ya walivyo. 

Wanaopenda kusema bado najipanga huwa wanasubiria wawe na vingi ili waanze.

Huwa wanasubiria kila kitu kiwe sawa ili wachukue hatua.

Hawaanzi biashara kwa sababu bado wanajipanga, hawaongezi Elimu, bado wanajipanga.

Hawajaanza Kilimo wanachotaka bado wanajipanga.

Kujipanga ni kuzuri ila UKIPITILIZA hugeuka SUMU inayokuua taratibu.

Kuja kushtuka - Wameshaoa, Wana watoto, Uzee umeingia na mwisho wanaona wameshachelewa hakuna wanachoweza KUBADILISHA.

Wanabaki KUJUTIA!

Na wewe vipi, BADO UNAJIPANGA? Niandikie maoni yako katika sehemu ya comments hapo chini

Post a Comment

0 Comments