USIOGOPE NDOA

Vijana wengi wa siku hizi huogopa kuoa au kuolewa kwa sababu nyingi. Wengine huogopa kupoteza uhuru wao, wengine huogopa gharama ya kutunza familia. Wengine wanasema wanaweza kupata raha zote za ndoa bila kujifunga katika ahadi za ndoa.  
Sasa leo nimekuletea somo hili fupi ambalo litakutoa hofu kuhusu hofu ya kuingia Kwenye ndoa

Nini maana ya ndoa?

Ndoa ni muungano kati ya mwanamke na mwanamume kuishi pamoja kama mume na mke muda wote wa maisha yao. (Sheria ya ndoa mwaka 1971 kifungu cha 9).

i) Wanaooana wawe wamekubaliana pasipo kulazimishwa na mtu.

ii) Ndoa ni ya mwanamke na mwanamume.

iii) Ni ndoa ya kudumu maishani.

Mpango na utaratibu wa MUNGU kwa wanandoa umewekwa wazi katika kitabu cha Mwanzo.

“Bwana MUNGU akasema si vema mtu huyu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufafana naye”. Mwanzo 2:18.

Hapa tunaona kuna suala la mamlaka katika ndoa, kwamba mke ni msaidizi.

“Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja”. Mwanzo 2:24.

Hapa tunaona kusudi la MUNGU katika suala la kuachana na kuambatana. Wanandoa wanatakiwa kuachana na wazazi wao katika maeneo matatu.

i) Kimwili; wawe na makazi yao wenyewe

ii) Kihisia; wategemeane na kutiana moyo na kusaidiana

iii) Kiuchumi; wajitegemee kwa mahitaji yao ya kila siku.

SABABU ZA KUITOA HOFU YA KUINGIA KATIKA NDOA

Ndoa ni chanzo cha heshima

''Ndoa na iheshimiwe na watu wote, malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu''(Ebr.13:4)            
    
Ndoa ni kitu halali kilichoanzishwa na Mungu katika bustani ya Edeni. 
''Anayempata mke amepata bahati njema, hiyo ni fadhili kutoka kwa Mwenyezi-Mungu.''(Mit. 18:22)            
  • Siku ya harusi ndiyo siku ya uhuru maishani, siyo siku ya kupoteza uhuru, kama wengine wanavyodhani. 
  • Wanandoa wanao uhuru wa kusaidiana na mwanzake bila woga. 
  • Wanao uhuru wa kupendana na mwanzake pasipo woga. 
  • Wenye ndoa wanao uhuru wa kubusiana, kukumbatiana na kujamiiana bila hofu ya watu wengine. 
  • Makapela hawana uhuru wa kufurahia vitendo hivyo mbele ya watu wengine pasipo woga. 

Kuhusu gharama za maisha
watu wawili wakichuma mali pamoja na kula kwenye sahani moja gharama za maisha huwa ndogo zaidi. ''Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watampinga: wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi.''(Mhu.4:12) hivyo mume na mke wenye juhudi zaidi wakishirikiana kiuchumi na kuweka Mungu mbele, watamudu maisha ya furaha pasipo shida.       
              
OMBI LANGU LEO  
Mungu asaidie vijana katika chaguzi la wachumba. Kila kijana apate mchumba mcha MUNGU na Ambaye watafikia malengo ya kufunganaye ndoa.               


Andika comment yako hapa

Post a Comment

0 Comments