Uchunguzi wa hivi karibuni uligundua kuwa zaidi ya 70% ya watu wanatamani wajasiriamali.Hii ni kutokana na vigezo vingi ambavyo kila mmoja kwa binafsi anavyo.Miongoni mwa vigezo hivyo ni uhuru wa maamuzi kuhusu hatima ya maisha yako mwenyewe.
Kwa nini unapaswa kuwa mjasiriamali?
Kuna sababu nyingi zinazosabaisha watu kupenda na kuanza ujasiriamali.
1. Uhuru
Kuendesha biashara yako mwenyewe inakuwezesha kuwa na malipo unayoyataka mwenyewe.Watu wengi wanaoendesha biashara zao wenyewe huwawezesha kuwa na kazi ambayo ni ya kujitegemea.
2. Fursa
Ujasiriamali unaweza kukufungulia ulimwengu mpya wa fursa kwako.Utakuwa na fursa ya kufanya chochote unachotaka katika maisha.Hii inamaanisha unaweza kuchagua kutumia maisha yako kubadilisha ulimwengu kuwa sehemu bora Zaidi,pia itakusaidia kuishi aina ya maisha unayotaka.
3. Matokeo makubwa
Watu wengi wanafanya kazi kwenye makampuni wasiyoyamiliki na wanafanya kazi kwa bidii ili kusaidia kampuni hiyo kukua na kufanikiwa.Ukitumia nguvu hiyo hiyo kuendesha biashara yako mwenyewe kila kitu unachofanya kitaathiri moja kwa moja biashara yako.
4. Uhuru
Hili ndiyo jibu la watu wengi watakupa ikiwa utawauliza kwa nini wanataka kuwa wajasiriamali.Kufanya kazi kwa kusimamiwa ni jambo ambalo watu wenmgi hawalipendi hivyo kuamua kufanya kazi au biashara zao wenyewe.
5. Wajibu kwa jamii
Unapoendesha biashara yako mwenyewe una uwezo wa kuwajibika kwa jamii na kufanya biashara yako kwa njia ambayo unafikiri inapaswa kuendeshwa.Hii ni kweli hasa ikiwa una hamu ya kuwasaidia wengine au ulimwengu kwa ujumla.Ikiwa unafanya kazi kwa mtu mwingine huenda usiwe na uwezo wa kuufanya ulimwengu kuwa sehemu bora zaidi kwa njia unayotaka.
6. Kuwa Boss wako mwenyewe
Hili ni jibu lingine la kawaida kwa nini watu wengi wanataka kuwa wajasiriamali.Ikiwa wewe ni bosi wako mwenyewe unaweza kufanya mambo vile unataka mwenyewe.Unaweza kufanya maamuzi yako mwenyewe,kuchukua hatua zako mwenyewe na kuamua hatima yako mwenyewe.
7. Kupata Wakati na Familia
Kutegemea malengo yako maalum katika maisha,kuwa mjasiriamali kunaweza kukupa uhuru wa muda na kukuruhusu kutumia zaidi mda wako na familia yako.
8. Kujenga urithi wa kudumu
Kazi nyingi huwapa wafanyakazi fursa finyu ya kutengeneza urithi wa kudumu kwa ajili ya familia zao.Lakini kufanya biashara yako mwenyewe kunaweza kukusaidia kufanya hivyo.
9. Kufanikiwa
Ikiwa una malengo maalum ambayo ungependa kuyakamilisha katika maisha yako,basi kupitia kuendesha biashara yako mwenyewe kunaweza kukusaidia kufanya hivyo.
Nini kinahitajika ili kuwa mjasiriamali?
Kuna faida nyingi za kuwa mjasiriamali,lakini sio kazi rahisi kuanzisha biashara na kuweza kuisimamia vema.Ila ukiamua kuchukua hatua na kufuata ndoto zako basi unaweza kufanikiwa sana katika ujasiriamali.
Sifa za wajasiriamali waliofanikiwa:
• Huwa shauku ya mafaniko
• Uwezo wa kusimamia hofu zao.
• Huwa na maono mazuri
• Kujiajiamini
• kuamini kuwa kila kitu kinawezekana
• Risk takers.
• Wabunifu
• Wavumilivu
• Ni kiongozi
• Ni washindani wasiokata tamaa
Ikiwa una sifa hizi,au unaweza kuzifuata sifa hizi basi wewe ni miongoni mwa wajasiriamali wenye mafanikio makubwa wanaokuja.
Mambo mengine mjasiliamali anapaswa kuyazingatia
Kuzingatia malengo yako
Ili ufike mbali inatakiwa ujiwekee malengo ya kuyakamilisha kila siku.Na siku husika hakikisha unakamilisha mambo yote uliyopanga kuyamaliza.
Ujasiri wa kukabliana na changamoto
Huu ni Uwezo wa kukabiliana na changamoto bila kuharibu malengo yako.
Usimamizi imara
Ili Kampuni iweze kufanikiwa inahitaji watu sahihi wenye uwezo wa kuongoza na kusimamia vema kampuni.Wajasiriamali waliofanikiwa wanajua jinsi ya kusimamia vizuri biashara zao.
Mtazamo wa muda mrefu
Ni rahisi kuzingatia mambo yale ambayo kampuni inahitaji kufanya katika siku kadhaa au wiki kadhaa zijazo.Ili kufanikiwa ni vizuri kupanga mikakati ya miaka kadhaa mbele.
Uuzaji
Bila kujali aina gani ya kampuni unayoendesha,unahitaji kuwa na uwezo wa kuuza maono yako kwa wengine ili uweze kupata mafanikio.Wajasiriamali wanahitaji ujuzi mkubwa wa mauzo.
Kujitegemea
Hii ni moja ya mambo muhimu zaidi mjasiriamali anapaswa kuyajua.Ni muhimu kwa mmiliki wa biashara kuamini kwamba anaweza kujitegemea.
Wajasiriamali lazima waweze kujifunza kutokana na makosa yao na kutafakari juu ya yale waliyojifunza katika maisha.
Kujifunza
Wajasiriamali wengi waliofanikiwa hawachoki kujifuza wakati wote.Ili kufanikiwa katika ndoto zako za ujasiriamali unapaswa kujifunza kutoka kwa wengine.Njia bora ya kujifunza ujasiriamali ni kujifunza ujuzi wa wajasiriamali waliofanikiwa na kisha kukuza ujuzi huo.
Usikose sehemu ya pili
0 Comments