Kati ya mambo ambayo yanafanywa sana na watu bila ya kujua gaharama yake ni hili la kufanya agano la ndoa madhabahuni na huku kiumbe kikiwepo tumboni.
Imekuwa kama ni jambo la kawaida sana kufanya kitu cha namna hii. Watu wanafunga ndoa na kabla ya kutimia miezi tisa tangu wapolifunga ndoa basi mtoto anazaliwa,ikiwa na maana ya kwamba, wakati wanafunga ndoa tayari kulikuwa na kiumbe tumboni.
Sasa ngoja nikushirikishe mambo kadhaa hapa chini;
1. Mtoto akiwa tumboni ana uwezo wa kusikia.
Mtoto anapokuwa tumboni anasikia kabisa ndio maana kuna vitu anaweza akajifunza akiwa tumboni ambavyo akija kuzaliwa vitaonekana kwenye maisha yake.
Mfano wa 1: UONGO TANGU TUMBONI
Zaburi 58:3 Wasio haki wamejitenga tangu kuzaliwa kwao; Tangu tumboni wamepotea, wakisema uongo.
Hapo unaona tabia ya UONGO ilivyoanzia tumboni.Inawezekana wakati mama zao wamebeba ujauzito walikuwa wanashinda maeneo ambayo kulikuwa kunaongelewa mambo ya uongo hivyo wakawa wanasikia na wao wakajifunza.
Walipozaliwa nao wakawa ni watu wa kusema uongo.
Mfano wa 2: Ugomvi wa Esau na Yakobo wakiwa tumboni
Wakati Rebeka anashangaa mapambano anayoyasikia tumboni kwake akiwa amebeba mimba,Mungu alimwambia hivi;
Mwanzo 25:23 BWANA akamwambia,
Mataifa mawili yako tumboni mwako,
Na kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni mwako. Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili,
Na mkubwa atamtumikia mdogo.
Ukisoma hapo, unaona kabisa kwamba hawa watoto walikuwa wanagombana wakiwa tumboni na mama yao akawa anahisi yale mapambano. Sasa rudi kwenye maelezo niliyokuambia hapo mwanzo kwamba watoto wakiwa tumboni wanakuwa na uhai kabisa ndio maana hapo walikuwa wanagombana tumboni.
2. Kile kinachoendelea mtoto akiwa tumboni ndicho kitakachokuja kutokea kwenye maisha yake atakapozaliwa.
Hapo kwenye Zaburi 58:3- Uongo ulioanzia tumboni ,ulienda kwenye maisha yao baada ya kuzaliwa.
Kwa habari za Esau na Yakobo ambao walikuwa wanagombana wakiwa tumboni ,walipokuja kuzaliwa ugomvi uliendelea kwenye maisha yao vile vile.
AGANO LA NDOA NA KIUMBE TUMBONI
Nikirudi kwenye somo hili,mwanamke na mwanaume wanapofunga agano la ndoa madhabahuni wakati mtoto yupo tumboni, maana yake ni kwamba MTOTO NAE ANAFUNGISHWA AGANO.
Maneno wanayotamka wakiwa madhabahuni huwa yanaenda kwa mtoto pia aliyeko tumboni.Tumeona hapo juu.
Mtoto aliyeko tumboni kama atakuwa na jinsia ya kike maana yake ni kwamba anafunga pia agano na Baba yake ,na kwa mtoto wa kiume pia anakuwa anafunga agano na mama yake.
Yaani ni agano la mzazi na mzazi na pia ni agano la mtoto na mzazi.
Matokeo yake ni kwamba,mtoto akija kuzaliwa huwa anajikuta anasumbuliwa na roho ya kutaka kuzini na mzazi wake kabisa kabisa kwasababu ya agano lililofanyika madhabahuni.
Au
Mzazi anajikuta anasimbuliwa na roho ya kutaka kuzini na mtoto wake wa kumzaa kwasababu ya lile agano alilofunga.
Iwapo kijana(wa kiume au wa kike) ataendelea kusumbuliwa na hiyo roho ya zinaa ndani ya damu yake ,itafikia hatua ambapo atajikuta amezini na mtu mwingine wa tumbo moja.
Haya mambo ni halisi kabisa na kuna familia zinazopitia mazingira haya. Mimi nimeona.
Haya mambo nimeyaona kwa watu yakiwatokea pale wanaponishirikisha matatizo waliyonayo ili kupata msaada wa ushauri na maombezi.
Kuna watu wamepitia haya maisha.
Biblia haielezi sana kwa habari za kuoa kwa Lutu,lakini tunaona tu namna Binti zake walipoingiwa na roho ya zinaa na kutaka kuzini na Baba yao mzazi na wakafanya hivyo na pia wakapata mimba.(Mwanzo 19:30-38).HAYA MAMBO NI HALISI KABISA.
Nimeona mahali ambapo unakuta kijana anakushirikisha kitu kinachomsumbua, Mtumishi unashangaa kitu anachokuambia.
Unaweza ukafikiri anatania lakini kumbe yupo kwenye taabu sana.
Sasa kama kijana akizaliwa katika mazingira kama hayo, zinaa itamsumbua sana kwenye maisha yake kutokana na lile agano alilofungishwa, na pia KUOA AU KUOLEWA INAKUJA KUWA TAABU SANA, kwasababu anakuwa amefungishwa agano lingine la ndoa wakati yuko tumboni.
Watu wengi wanafanya haya mambo ya kufunga agano la ndoa madhabahuni na huku mtoto yuko tumboni kwasababu tu hawajui GHARAMA YAKE ILIVYO KUBWA.
#USHAURI
Ni heri kutokwenda madhabahuni kufunga agano la ndoa wakati kiumbe kipo tumboni tayari, kuliko gharama zilizopo baada ya hapo.
Ni bora kuja kufanya utaratibu mwingine wa matengenezo ya ndoa kulingana mfumo wa Kanisa husika.
Ni bora mtoto aliyezaliwa tu nje ya ndoa moja kwa moja kuliko ambaye wazazi walienda kufunga agano la ndoa madhabahuni wakati yuko tumboni. AGANO SIO KITU CHA MCHEZO.
Siku za hapa katikati hili jambo litasumbua sana watu kwasababu nyakati hizi ndoa za madhabahuni ni nyingi zaidi tofauti na miaka ya nyuma LAKINI tatizo ndio hilo la kuwepo tayari kwa viumbe tumboni.
Ni ndoa chache siku hizi ambazo hazipiti kwenye hili tatizo.
Kitu kibaya zaidi ni kwamba, mtoto anaingizwa kwenye agano la kwamba HADI KIFO KITUTENGANISHE.
Asante Sana
Nimebarikiwa na Ujumbe huu ndani yangu
Nimebarikiwa na Wewe Usomaye Ujumbe huu
Ni maombi yangu kwa Mungu kwa Roho wake akufunulie zaidi jambo hili lilivyo.
1 Comments
Jamii inazidi kuelimika kupitia kazi zako moto moto zinazolenga kuibadiri jamii usichoke kutuelimisha na kutujuza mambo mengi zaidi
ReplyDelete