TAFAKARI UJUMBE HUU KWA MAKINI🙏

Nimeichukua mahali fulani, 

Shikamoo dada Irene Mbowe.
Nimesoma ushuhuda wako wa Duka la samaki nikakumbuka mm ushuhuda wangu.
Mwaka 2015 Mwezi wa Saba nilikutana na Changamoto moja ambayo sikujua MUNGU Ananiepusha na balaa. Ilikuwa hivi .
Nilipata Mchumba ambaye alinipenda sana. Katika mahusiano yetu akawa muaminifu sana. Na nikamuamini sana Urafiki wetu ukadumu kwa miezi. taktibani tisa. Akiwa ananipenda na tunapendana sana.
Na tukakubaliana Kabisa kwamba muda wa kupeleja posa umefika.
Irene kijana akinipenda mpaka wenzangu wakanionea Wivu. Yale mambo kumi uliyotasema yooote alikuwa nayo da Irene.
Ilikuwa lazima aamke saa kumi na Mojaa asbh aniamahe na mimi. Kisha Tuombe pamoja,Alafu baada ya hapo aniambie amka ruka kamba,Yani nifanye mazoezi walau nusu saa. Na akitaka nimpigie picha aone. Baada ya Hapo angeniambia ratiba yake ya siku nzima. Alinipenda sana da Irene.
Zawadi nzuri nzuri akinipatia za kila aina.
Akiniheshimu na alinihakikishia kabisa kwamba hana msichana mwingine na hahitaji msichana mwingine.
Irene kwangu nikaamini.
Maisha yakaendelea. Kanisani wakajua tu wachumba.
Ofisini wakajua kabisa mimi na Baraka ni wachumba. Mpaka wakawa wananiita Mrs Baraka.

Baraka akanifuata na kuniomba akajitambulishe kwa wazazi. Sikuona shida yoyote. Hapo uchumba una mwaka na.mwezi mmoja.
Siku nimeshaongea na mama yangu kuhusu mchumba kwenda mama akafurahi sana.
Na wakajiandaa nyumbani maana mchumba anakuja.
Nakumbuka nilitoa na.pesa chooo kitengenezwe vyema. Basi, Maandalizi yakakamilika.
Nikawa niko nampigia Baraka.simu hapokei. Napiga hapokei. Mara hapatikani kabisa. Nikaanza kupata wasi wasi. Kuna nini kimetokea?Nikampigia Rafiki yake. Akapokea lakini hana la kuniambia. Tangu saa sita mchana tunasubiri ugeni.
Saa nane ,tisa,kumi,Kumi na moja olaaaa.
Nilioaniki sana na kuanza kulia.
Simu ya Baraka mwisho akaizima kabisa.
Rafiki yake nikamuuliza kuna nini?Akaniambia utakuja Bwana kuongea naye. Nikamuuliza kuna.shida akasema utaongea naye mwenyewe.
Irene nilipaniki. Nililia sana. Sikuweza hata julala ule usiku Irene. Maana mtaa mzima ulijua Napeleka mchumba kutambukisha na kuvishwa pete. Niliumia ssna. roho ikaniambia labda kapata shida.
Nikakesha usiku kucha. Asbh nikapanda basi kurudi mjini.
Sikwenda kabisa kazini wiki nzima.
Baraka akaanza kutopatikana,Mara hapokei simu. Mara apokee haongei kitu cha kueleweka.
Kwa vile kwake napafahamu nikaona isiwe shida. Nikamfuata.
Irene sikuamini nikichokuta. Nilimkuta Baraka yuko na kaptula yake. Amekaa Sebuleni.
Kwanza wakati naenda nilipiga honi sana lakini hakuna.aliyetoka kunifungulia geti. Na nikiwa njiani nilimoigia kumwambia nakuja. Akapokea simu akasema poa.
Nukafika hakufungua geti wakati siku zingine ananifungulia.
Nikafungua mlango mdogo maana funguo ninazo.
Nikawa natembea. Kufika karibu na mlango wa sebuleni nikaona nje kwa nyuma nguo zimeanikwa mpaka.za kike. Moyo ukafanya kushtuka. Lakini nikasema labda ndugu yake. Lakini hana tabia ya kukaa na ndugu.
Kufika Sebueni nikasikia akiongea na msichana wanacheka. Nikashtuka sana .Nikajikaza nikaingia sebuleni.
Nikamkuta kakaa kwwnye sofa anawatch Tv. Akanisalimia kwa dharau. Kisha akasimama kwenda jikoni kama kumfuata yule msichana.
Akaongea naye. Sijui akimwambia nini. Yule msichana akatoka akaniambia mambo,Alafu akaingia ndani.
Niliitika poa. Mambo.. akasema poa.
Nikawa na maswali mengi ya kumuuliza Baraka,Kwa nini hakuja nini kilimpata?
Lakini oia huyo.msichana ni nani?Nilitamani anijibu haraka sana kabla hata sijamuuliza nilitamani niwe na majibu.
Nilikuwa nimesimama bado.. Kaa,Mbona hukai?Akiniuliza.
alionekana wala hajali.
Nikamuuliza Mbona hamkuja tena?Mlipatwa na nini?
Akaniambia kaaa,Usiongee na mimi ukiwa umesimama.
Nilitii nikakaaa. Akatabasamu akasema,Nakupendea tuuu jinsi una moyo wa kutii. Uendelee na moyo huo huo mamii. Akacheka tena.
Ni kwa kejeli aliniambia. Nikamuuliza tena mbona hamkuja?
Akaniambia,Nimeahirisha uchumba wangu na.wewe. Niliona hunifai tena.
Unasemaje?Nilifoka.. . Unasemaje?
Aliniangalia na kunikazia macho kisha akasema,
Weee.. shika adabu yako. Unamfokea nani?Unamfokea nani?
Alikaza sauti na kunikaripia sana,akionyesha kukerwa na nilivyomng'akia.
Ni kama nilishikwa na Butwaa fulani hivi.
Amepatwa na nini?Nilijihoji.
Nini kimemsibu huyu kaka?
Nikiwa bado nashangaa machozi yananitoka.
Baraka,Umepatwa na nini?Nilijikuta nakuwa mpole sana.
Lakini moyo wangu ukiwa na maumivu makali.
Tangu mwanzo unanipigia simu,Unafungua geti,unaingia ndani najua wewe ni mwanamke mpole sana na muelewa sana. Na kama unakumbuka nilikuambia huwa sipendi ugomvi. Na maamuzi yangu napenda yaheshimiwe. Hilo unalijua sio?
Aliniuliza,
Najua nini?
Najua nini?Nilimfokea tena. maana alionyesha kunidharau.
Nikaanza sasa kufoka.
Akaniambia foka ukimaliza ondoka kama ulivyokuja.
Sikuamini. Nikamwambia ahaaaa, Ni huyo msichana anakupa.kiburi eee nikasimama ili kuelekea chumbani.
Akaniita,Sara,Sara,Sara huku bado naendelea kutembea.
Nilipofika mlangoni nikashika mlango wa chumbani umefungwa. Yule msichana kjifungia ndani. nikashika kitasa kwa nguvu kukigusa gusa lakini hakifunguki.
Baraka akacheka akaniambia,
Unataka kufanya nini?
Mimi na wewe basi. Ndio mahusiano yameisha mama.
Irene sikuamini. nilikaa sakafuni nililia kama mama aliyefiwa na mtoto wake. Nilipata uchungu mkali sana Irene. Mkali mnoooo.
Alinifuata pale sakafuni akanishika mkono akaniburuza mpaka sebuleni. Irene kiliniuma.siwezi kukuelezea.
Akanifukuza kama mbwa. Kwenye nyumba ambayo nilikuwa nashinda kuotesha maua,miti,matunda.
nyumba ambayo alikuwa ananiuliza mamii tufanyeje hapa,Ramani tulishirikiana kuichora.
Ananiambia hapa jikoni kwako unataka paweje, vgunba vya wanao nk.
Aisee ile siku ilikuwa motoo mkali sana.
Nikajikongoja. nikaenda kwangu. Nikafika nikalia sana.
Rafiki yangu Eva na Salome wakaja kunishauri na kunitia moyo lakini wapi.
Nilikonda kwa kulia. Nikachakaaa.
Baada ya miezi mitatu Baraka akamtolea yule dada posa. akamuoa. Nikapata tena uchungu moyoni. Safari hii nikalazwa kabisa. hoi mgonjwa.
Basi yule kaka akaoa mke wake. wakaanza maisha yao ya Ndoa.
Ilibidi nibadilishe mpaka njia da Irene. na mpaka ikafika mahali nikaomba uhamisho kikazi. nikahamia mkoa mwingine maana nilikuwa naumia sana nikikutana na.watu wanaonijua,aofisini kila mtu alinihurumia. mpaka Bosi.
Basi.
sikujua Mungu ananiepushia jambo.
Baada ya muda nikasikia Baraka kashikwa ana kesi ya wizi. Kumbe zile mali zake na kila kitu chake alikuwa ni mwizi. Na alikimbia akawa anatafutwa. Akahonga honga sijui lakini kesi ikatulia tuu.
mwisho wa siku akashikwa.Kesi ya wizi. akahukumiwa kifungo cha mamiaka.
Mali zake.zoote.zikataifishwa. Yule mke wake ikabidi aondoke aende.kwa wakwe zake.
Niliposikia yale niliumia tena nikamhurumia. na ndipo nikajua MUNGU Akiniepushia jambo kubwa sana.
Nilienda magereza nikamkuta maskini kachokaa sana. Hana afya,ana mawazo na hana hata mtu wa kumsalimia. Aliponiona alitoa tuu machozi na kuniangalia wala.asiseme neno. nilimhurumia pia. sana.. nilimwambia tuu pole sana. yatapita.
akaniambia miaka 30 jela sio.michache.
nilimhurumia sana.
Nikaondoka. ikanichumua miaka 2 mizima bila mahisiano. Mwaka jana nikapata mchumba. tukaoana.


Post a Comment

0 Comments