MANENO YATOAYO MACHOZI KUTOKA KWA MZAZI



💘"Mama anaongea na mwanawe na kumpa ​Usia"​

💘Mwanangu mpenzi:

💘Kuna siku utanikuta uzee, sitafanya mambo yangu kwa akili;

💘Yakitokea hayo nakuomba tafadhali nipe muda na ​subira ili unifahamu !!​

💘Pale mikono yangu itakapotetemeka, na chakula changu kikaangukia kifuani pangu, na nisipoweza kuvaa nguo zangu;

💘Jifunge na ​kusubiria, na kumbuka miaka imepita nilikuwa nakufunza ambayo leo siwezi kuyafanya!!​

💘Ikiwa leo si maridadi na sina harufu nzuri; usinilaumu.. kumbuka udogoni kwako nikijitahidi sana nikufanye uwe maridadi mwenye harufu nzuri!!

💘Usinicheke utakapoona ujinga wangu na
kutofahamu mambo ya wakati wenu huu, lakini wewe kuwa jicho na akili yangu ili niyapate niliyoyakosa!!

💘Mimi ndiye niliyekufunza adabu na mimi ndiye niliyekufunza vipi ukabiliane na maisha;

​💘Sasa inakuaje leo unanifundisha yaliyo wajibu na yasiyo wajibu?​

💘Usinichoke kwa udhaifu wa kumbukumbu yangu, na uchelewaji wa ​maneno yangu na fikra zangu​ wakati ninapozungumza nawe, kwani furaha yangu wakati huu ni kuwa pamoja nawe tu!!

​💘Wewe nisaidie tu kupata ninachohitaji;​ kwani bado najua ninachotaka!!

💘Miguu yangu ikikataa kunipeleka sehemu ninayotaka kwenda; ​nihurumie​ na kumbuka kwamba mimi nilikushika sana mkono ili uweze kutembea!!

​💘Usione haya abadan kunishika mkono wangu leo;​ kwani kesho utatafuta wa kukushika mkono wako!!

💘Katika umri wangu huu; elewa kuwa mimi siyaelekei maisha kama wewe; lakini kwa ufupi nangojea mauti; kwa hiyo ​kuwa pamoja nami wala usinitupe!!​

💘Pale ukikumbuka makosa yangu; jua kuwa mimi nilikuwa sitaki ila maslahi yako!!

💘Na mimi napenda sana unayonifanyia hivi sasa kwa ​kunisamehe matelezo yangu na kusitiri aibu zangu..​

​💘💘NAWE MOLA AKUGHUFIRIE NA AKUSTIRI!!💘💘​

💘Bado ​vicheko na tabasamu zako vinanipa furaha​ kama ulivyokuwa mdogo...
kwa hiyo usininyime suhuba yako!!

💘Nilikuwa nawe wakati ​unazaliwa;​ kuwa nami pale ​nitakapofariki!!​

​💘Maneno bora yaliyopitia katika maisha yangu, na hata nikiyarudia mara elfu moja sichoki kuyasoma..​

Hayo ndio niliyoyaona mimi, kama nawe unayo maneno mengine, shuka chini ya huu ukurasa kisha bofya sehemu iliyoandikwa post a comment kisha tuandikie maneno mengine ambayo akiyasema mzazi kiukweli inaumiza.


Post a Comment

1 Comments

  1. Mungu wangu warehemu wazazi wangu na uwahurumie kama walivyoo nihurumia Mimi nilipokuwa mdogo.

    ReplyDelete
Emoji
(y)
:)
:(
hihi
:-)
:D
=D
:-d
;(
;-(
@-)
:P
:o
:>)
(o)
:p
(p)
:-s
(m)
8-)
:-t
:-b
b-(
:-#
=p~
x-)
(k)