JE, TUFANYE NINI BASI



Ni jambo la muhimu wakati tunapokumbana na jambo tusilo lijua au kuwa na hakika nalo kutafuta mwongozo; Je tufanye nini na au tufanyeje...?  

Ni vyema kuomba mwongozo badala ya kukurupuka kufanya jambo  kimazoea, au kwa kufuata mkumbo, na kuishia kupata matokeo yasiyo tosheleza au kutokufanikiwa kabisa.

Tunapokumbana na magumu katika maisha vilevile, ni jambo la muhimu kuomba mwongozo kutoka kwa Mungu wetu, Je tufanyeje? badala ya kumwambia Atufanyie yeye....

Swali la tufanye nini? aliulizwa Yohana mbatizaji na umati wa watu, kisha watoza ushuru, na hata askari, kufuatia mafundisho yake (Luka 3:10-14)

Yesu nae alikumbana na swali hilo mara kadhaa; .... mwalimu mwema, nifanye nini nipate ku urithi Uzima wa milele? (Luka 18:18-30).

Pia makutano walipo sikia mafundisho yake, walimuuliza; tufanyeje ili tupate kuzitenda kazi za Mungu? ( Yohana 6:28‬) 

Petro alipo hutubia mkutano na watu waliposikia mafundisho yake walichomwa mioyo yao, waka mwambia yeye pamoja na mitume wengine; tutendeje ndugu zetu?( Matendo 2:37)

Paulo nae alipo tokewa na Yesu alipokuwa safarini kwenda Damascus kuwatesa Wakristo, alimwuliza Yesu; ... nifanyeje, Bwana?....

Ukitazama katika nukuu zote hizo hapo juu, utaona kila swali lilipewa jibu la aina yake hata kama baadhi ya maswali yalilenga jambo lile lile.

Pili, maswali haya,hayakuomba;  UTUFANYIE au NIFANYIE...

Waulizaji walikuwa na nia na shauku ya kutenda lakini hawakujua watendeje. Hivyo, kuomba kwao ni kutaka kuoneshwa nini cha kutenda na njia ya kutenda na sio kutendewa.  kwa kifupi waliomba mwongozo

Leo hii katika janga tulilo nalo, maswali yetu kwa Mungu yamekuwa ni maombi ya yeye kuliondoa janga hili badala ya kuomba Mwongozo wa ni nini cha sisi kukifanya.  

Mungu ametupatia AKILI, UTASHI, MAARIFA NA NGUVU za kutenda. Tunacho hitaji kutoka kwake ni mwongozo wa ni kitu gani cha kufanya. 

Bila shaka umewahi kuona mitandaoni video za watu wanao okoteza hela hewa, kutoka katika hewa na kuzijaza kwenye mapochi yao, eti wakiwa na Imani kuwa Mungu atajaza mle hela za kweli.

Sasa kama Mungu akijaza yale mapochi kwa hela, Je akili, maarifa, na nguvu ambazo Mungu amewajalia vitakuwa na umuhimu gani?

Hata sisi leo hii na tukamwombe Mungu atupe mwongozo wa kutenda tukapate kupambana na magumu tuliyo nayo. Ikiwa kama vita ni vyake, basi atatujibu (2 Nyakati 20:17).

Niite nami nitakuitikia. Nitakuonesha mambo makubwa na magumu usiyo yajua (Yeremia 33:3)

Post a Comment

1 Comments

  1. Tumuombe mungu atupe neema na busara za kutambua na kufanya maamuzi sahihi pale tunapojiuliza Tufanyaje?

    ReplyDelete
Emoji
(y)
:)
:(
hihi
:-)
:D
=D
:-d
;(
;-(
@-)
:P
:o
:>)
(o)
:p
(p)
:-s
(m)
8-)
:-t
:-b
b-(
:-#
=p~
x-)
(k)