WEWE NI DHAHABU

Watu wengi sana wamepoteza HAMASA ya maisha kwa sababu wameruhusu THAMANI yao itokane na MAONI ya watu wengine.Niliwahi kusoma mahali maneno ya HEKIMA yaliyosema “THAMANI yako HAIPUNGUI kwa sababu ya MTU kushindwa KUIONA”(Your Value Doesn’t DECREASE Based on Someone’s INABILITY to see It).

Kuna watu wengi sana HAWATAONA thamani ya WAZO lako na watakuambia halitafanikiwa.Kuna watu wengi wataonyesha dharau kwa KIPAJI chako,ila haimaanishi kuwa hakina thamani.Kuna watu wataibuka na kusema MANENO ya kukuonyesha wewe si wa MAANA kabisa.Kuna watu hawataona thamani ya NGUVU na KUJITOA kwako unakofanya ili kuwasaidia,kuna watu hawataona thamani yako kama KIONGOZI na wataona hakuna ulichofanya n.k
KWA MAHITAJI YAKO YA


WEBSITES DESIGNING AND DEVELOPMENT, MOBILE APPS BUILDING, GRAPHICS DESIGNING, VIDEO EDITING AND CREATIVITY......CONTACT US +255 743 524 143/+255 657 014 782


MBIFILE CREATIONS...


Kwenye maisha watu wa namna hii hawataisha,utakutana nao NYAKATI mbalimbali.Kitu cha Muhimu cha kukumbuka ni kuwa THAMANI ya DHAHABU huwa HAIPUNGUI kwa KUISEMA VIBAYA au kwa KUITUKANA.Dhahabu haijisikii vibaya inaposemwa wala haitafuti KUJITETEA kwa sauti INAPOTUKANWA.Nguvu ya dhahabu iko kwenye KUJITAMBUA na KUBAKIA kuwa ni dhahabu bila kujali nani KASEMA nini juu yake.

Ili ubakie na nguvu ya kiwango cha DHAHABU lazima kwanza ujue wewe ni dhahabu.Usikubali MANENO ya wanaotaka kukuonyesha HAUWEZI au HAUFAI yakukatishe TAMAA na KUKURUDISHA NYUMA.Hata kama HAWAONI thamani yako,anza siku kwa kujiambia “MIMI NI DHAHABU,THAMANI YANGU NAIJUA


Post a Comment

0 Comments