JIFUNZE KITU KUTOKANA NA MTEGO WA PANYA


Baada ya mwenye nyumba kuona panya anasumbua kwa kula nafaka zake, aliamua kununua mtego na akamtega.

Panya lile jambo lilimpa huzuni, akapiga mbiu kuwatahadharisha na wengine akina kuku, mbuzi ,ng'ombe. waungane na kuutegua.


Alisikika akisema"Kuna mtego mwenye nyumba kaweka mtego jamani"

Kuku akahoji: "Mtego wa nini?"

Panya: akajibu "ni wa panya"!!

Kuku akasema huo ni mtego wa panya mimi unanihusu nini?

Ng'ombe na  Mbuzi nao wakajibu kama kuku alivyojibu... "Panya pambana na hali yako hilo tego halituhusu ni lako"

Basi panya hakupata msaada ilibidi ajihadhari mwenyewe kutokana na mtego huo.

Usiku mmoja nyoka alipita na akanaswa mkia na ule mtego.

Mwenye nyumba akajua mhalifu wake ashampata, akapeleka mkono gizani achukue mtego na panya alienaswa, akang'atwa na nyoka.

Mwenye nyumba akapelekwa hospitali kwa matibabu, wakati anaendelea na matibabu kuku akachinjwa kwa ajili ya kitoweo cha mgonjwa.

Baadae mwenye nyumba akafariki, mbuzi na ng'ombe wakachinjwa ili watu waliokusanyika kwenye ule msiba wapate chakula.

"Mtego wa panya"

Hapa tunajifunza nini?
1. Tusaidiane tukutwapo na shida
2. Tuache ubinafsi
3.Tatizo la mwenzako la leo laweza kuwa lako kesho.
4. Usifurahie mwenzio kupata shida
5. Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu

Pana masomo mengi sana hapoo!!


Post a Comment

0 Comments