Kuna kipindi rafiki yangu fulani ambaye huwaga ana aibu sana na ni mtu ambaye siyo wa kujiwakilisha na watu alikuwa na harusi. Sasa ilikuwa anatakiwa kukusanya watu wa kumchangia na kukusanya michango. Katika kipindi kile cha kutafuta michango ili kuwezesha harusi niliona kama rafiki yangu kabadilika kabisa na utadhani siyo yeye.
Kwanza amekuwa anaheshimu muda, yaani akiambiwa saa kumi uje uchukue mchango basi saa kumi kasoro tayari kashafika eneo la tukio. Lakini pia katika kipindi hiki alikuwa na bidii ya ajabu sana na alikuwa anajituma sana kufuatilia michango ili kufanikisha shughuli yake, alikuwa analala masaa machache sana.
Na zaidi ya yote kipindi hiki kile kitu kinaitwa aibu hakuwa nacho kabisa. Na kubwa kuliko alijikuta ni mtu anayeweza kujiwakilisha na watu vizuri sana bila hofu. Baada tu ya harusi kuisha yule jamaa akarudi akawa vile vile tena mvivu, mwenye aibu, hajali muda, anapenda kujitenga tenga.
Kuomba Ushauri))
Sasa kuna kipindi jamaa yangu huyu alipitia changamoto kubwa ya kifedha hivyo akawa ananiomba ushauri. Nikamwambia unakumbuka kipindi ulichokuwa unapambana kwaajili ya harusi yako, akajibu ndiyo, nikamwambia "Pambana kama ulivyopambana kipindi cha harusi yako".
Akakubali na baada ya muda akanipigia simu kuwa kwa sasa ameamua kuishi maisha yake yote kama alivyokuwa akiishi kipindi alichokuwa akielekea kufunga harusi.
Funzo))
1. Kujitoa Ufahamu.
Sasa nikajifunza kitu kikubwa sana kupitia maisha ya huyu rafiki yangu kipindi cha kuelekea harusi yake. Nikajua kuwa "Kama usipojitoa ufahamu basi huwezi kufanya vitu ambavyo hujawahi kufanya".
Kujitoa ufahamu namaanisha kuwa kufika hatua ya kufanya jambo bila kujali watu watasemaje na watakuonaje. Yaani wewe unafanya chochote ambacho unajua kinakupeleka kule unakotaka kwenda. Unafanya kitu kinachokupeleka kwenye malengo yako
2. Kuishi kwa kufanya mambo kwa "Deadline".
Ni hatari sana kuishi kama utaishi duniani milele. Watu wanaofeli kwenye maisha ni wale ambao wanaishi duniani kama wataishi milele. Wanaishi kana kwamba watakuwa vijana milele. Wanaishi kana kwamba watakuwa na nguvu milele. Wanaishi kama hawatazeeka.
Lakini watu wanaofanikiwa huishi kwa deadline. Wanajua umuhimu wa leo waliyonayo hivyo huwezi kuwashawishi kuhusu kufanya kesho linalowekekana leo. Watu wanaofanikiwa ni wale wanaouishi ule msemo usemao "Life is too short".
Ni lazima tujifunze kuishi kwa deadline, kuishi kwa kuitumia leo uliyonayo kwa kiwango cha juu
Rafiki yangu bwana harusi alipokuwa na deadline ya harusi alipambana kuhakikisha kuwa anatimiza kila kitu kinachotakiwa kabla ya siku ya harusi kufika. Hakikisha unaweka malengo yenye deadline. Jiwekee deadline ya kutimia kwa ndoto yako. Weka deadline ya malengl yako ya muda mrefu na muda mfupi. Usifanye vitu bila deadline.
MWISHO))
ISHI KAMA BWANA HARUSI MTARAJIWA KWA KUJITOA UFAHAMU ILI NDOTO ZAKO ZITIMIE NA KUWEKA DEADLINE YA KILA UNACHOFANYA
Nikutakie siku ya Deadline!!
0 Comments