Kijana mwenzangu najua unapambana sana kutoboa kwenye maisha ila nakupa kanuni za kufanikiwa.
1.HESHIMU KIPATO CHAKO
Leo huna hela umepata kidogo au umekosa kabisa.kwa heshima na tahdhima unaenda kwa mama nitilie unakula wali Nyama buku na maji ya bure unaenda kulala.maanake umetumia buku tuu umeshiba.
Siku umepata sasa hela. Unataka uende kwenye mkahawa mkubwa unanza na Supu ya kongoro elfu 2000 alafu ugali Nyama choma elfu 6 na maji makubwa ya elfu moja.ukitoka hapo bodaboda mpaka kwako.mb za buku mbili kuangalia YouTube ambayo haina faida yotote kwako.asubuhi Supu nzito umesahau mihogo na chai ☕️ nyeusi kama mimi au na maji ya chumvi. Heshimu kipato chako kidogo unajopata jifunze kufanya savings kila siku.
2.ACHA TAMAA ZA MWILI PENDA TAMAA ZA MAISHA.
Unapambana sana utopoe ila una foleni ya wanawake kama mchwa. Huyu anakupiga kizinga ya elfu kumi yule tano mwingine voja mara baby leo sijala ooo baby mjomba amekatwa na umbu naomba hela mara ooo nataka kwenda saloon na baby baby nyingi nyingi tuu ambazo hazina maana.
Sikia. Tafuta mwanamke ambae atakupa mawazo ya kimaisha.mwanamke ambae atakuambia baby naomba tufanye hili baby nunua kiwanja baby nipe mtaji ninunue nguo nitume home waniuzie baby leo tusile nyama wiki yote Hii tule majani kama mbuzi tusave hela.baby acha ninyoe nitasuka siku zijazo.baby pole kwa kazi nakupenda na busu la shavu mwaaaaaa.baby tupambane tuhamie kwetu mwaka huu. Kijana mwenzangu huyu mwanamke ukimpata ujue umepata almasi au dhahabu. Mshikilie sana maana atakufanya ueshimike sana.achana na wale wanaofuatilia seoson na umbea kwenye saloon. Kosa mshahara sio kuoa.
3.ISHI KWA MALENGO.
Jiweke malengo tena weka zile kubwa kubwa sio ndogo ndogo. Weka malengo ya mwaka weka malengo ya miaka mitano.pambana kuakikisha unatimiza malengo Hata kama sio zote bac walau tatu zitimie.usiogope kuanguka ukianguka nyanyuka tena kujikwa sio kuacha safari.na kukatwa na kisu haimanishi hutoitumia tena.pambana kutimiza malengo kwa kumuomba mungu na kupambana zaidi.never give up.
4.KUNG'UTA MARAFIKI FAKE.
Kijana mwenzangu ukiona marafiki zako mnakaa kijiweni Hamna Cha maana zaidi ya story za madem na umbea ujue umaskini unakukaribia taratibuuu. Chagua marafiki wa kutembea nao. Rafiki anaweza kukufanya ufanikiwe na vilevile anaweza kukufanya usifanikiwe kabisa.usiogope kuachana nao Kwani utakuwa umepiga hatua kubwa sana kwenye maisha yako.
5.WEKA USHINDANI.
Hivi leo una amka alafu unaskia rafiki yako au adui yako amenunua kiwanja au amejenga au kanunua ndinga kali utajiskiaje? Najua utaumia na kuwa na wivu. Huo wivu ifanyie kazi hakikisha na wewe unapambana mpaka unamfikia au unampita kabisa.huo tunaita wivu wa maendeleo. Ndo wivu mzuri kwa vijana saizi.
NAKUTAKIA KILA LA HERI KWENYE MABADILIKO YAKO
Sisi,
0 Comments