JUKUMU LA KUKESHA KULINDA KONDE LA BARAKA ZAKO NI LAKO MWENYEWE :



📚ANDIKO KUU: Mathayo 13:24-28.

24 Akawatolea mfano mwingine, akisema,
Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake ;

25 Lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.

✍️ KATIKA maisha yetu ya WOKOVU ni maisha kamili yenye maisha kamili ya kimungu.
Hivyo lazima maisha yetu ya Kiroho yastawi sambamba na maisha yetu ya Kimwili.

✍️Yesu Kristo anatoa mfano wa mkulima aliyelima bonde akapanda ngano,alipolala (hakulinda shamba)akaja adui akapanda magugu katikati ya ngano.

✍️ Hivyo katika bonde moja kukawepo Mbegu za aina mbili, NGANO na MAGUGU na vyote vikatoa matunda sawasawa na Mbegu yake.
Mbegu ya ngano ikazaa ngano na Mbegu ya magugu ikazaa magugu.

KATIKA SOMO HILI NATAKA TUJIFUNZE JUU YA KAZI YA YESU.

📖 Wakolosai 1:13.

" Naye alituokoa katika nguvu za giza,akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa mwana wa pendo lake".

Kristo Yesu anapoingia ndani ya mtu hufanya mambo matatu makuu.

[|] Anamwokoa toka nguvu za giza, Mauti na kuzimu.

[||]. Anatuhamisha toka katika ufalme wa shetani.

[|||]. Anatuingiza Katika ufalme wa Mungu.

✍️ Baada ya hatua hizi Yesu anatupa mamlaka za kifalme wa mbinguni.

📖 LUKA 9:1
"Akawaita wale Thenashara, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi".

📖 MATHAYO 16:18-19
" 18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro,na juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.

19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.

✍️ FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI tunazo katika Kristo Yesu.

✍️ Yesu anasema watu walipolala adui akaja apanda mbegu za magugu katikati ya mbegu njema za ngano.

✍️ MAOMBI ya ULINZI ni ya muhimu katika ustawi wa MAISHA ya Kiroho na Kimwili .
Mtu wa Mungu uliyeitwa kwa jina la Bwana, wewe ni mlinzi wa MAISHA yako, maisha ya watoto wako na mali zako.

✍️ MAISHA yako lazima yawe yameunganishwa (Connected) na madhabahu ya Mungu aliye hai.

FUNGUO za BARAKA,.
FUNGUO za ustawi wako,
FUNGUO za Mali zako,
Ziko mikononi mwako sio nje yako.

✍️ Kuokoka pasipo kudumu katika MAOMBI,utafungwa na NGUVU za giza na utafungika.
Utaanza kuangaika kutafuta maombezi.

✍️ MKRISTO usitegemee upako wa kununua, usitegemee upako wa SABUNI na CHUMVI Hapana!!.

UPAKO wa uweza wa Mungu unapatikana ndani mwa MAOMBI tu. LUKA 6:12-19

Wapo wakristo wengi MAISHA yao yamejaa kifusi cha MAGUGU,adui amefukia visima vyao vya Baraka,visima vyao vya UTAJIRI na HUDUMA.

BWANA asema lazima tujifunge silaha zetu tupigane vita.

Maana ingawa tunaenda katika mwili,hatufanyi vita kwa Jinsi ya MWILI.

Wale waliofungwa katika madhabahu za KICHAWI sharti wasimame na familia zao na mali zao mbele za BWANA.

Niishie hapo kwa leo.

Mungu wa mbinguni akupe nguvu ya kuendelea kukesha huku ukilinda konde la baraka zako.✍️.

Post a Comment

0 Comments