JINSI YA KUPIKA MUHOGO WA NAZI



Mahitaji
1.Muhogo kiasi.

2. Tuwi jepesi  kikombe 1 na nusu. 

3. Kitunguu maji.     1.

4. Tuwi zito kikombe.  1.

Jinsi ya kuandaa

➖Chukuwa muhogo wako menya vizur,na ukatekate vipande vidogo vidogo.

➖baada ya hapo chukuwa muhogo wako uweke katika sufuria, weka maji kiasi cha kuufunika muhogo na utaweka chunvi kiasi chako, hapo utauwacha muhogo wako kuiva kiasi.

➖baada ya hapo utauwepua muhogo wako usiuwache ukaiva sana,utahakikisha muhogo wako umekauka vizur kwa kuumwaga maji.

➖baada ya hapo weka tena muhogo wako katika sufuria,weka na kitunguu maji (1 cha kiasi), utaweka na tuwi lako jepesi (kikombe 1 na nusu) weka kiasi cha kuufunika muhogo na uwache muhogo wako uwive, hakikisha umekauka kiasi na utauwepua. 

➖baada ya hapo chukuwa tuwi lako zito ambalo ni (kikombe 1) utalipika adi kuwa zito zaidi na utaliepua.

➖baada ya hapo chukuwa muhogo wako, weka kwenye kibakuli chako na utachukuwa  tuwi lako zito kuurashia rashia kwa juu.

➖hapo muhogo wako utakuwa tayar kuliwa.

        
       TAMU: 🤗🤗

Post a Comment

0 Comments