SOMO -ZIFAHAMU FAIDA ZA KITUNGUU SWAUMU


- Kitunguu saumu ni mmea ambao unatumiwa kwa matumizi mbalimbali lakini kubwa ni kutumika kama chakula

- Kitunguu saumu kina faida nyingi za kiafya kwa vile kina virutubisho bora kwa ajiri ya ukuaji wa mwili

- Mbali na kuwa na virutubisho vingi kitunguu saumu pia kina dutu/kemikali adhimu ambazo zina uwezo wa kupambana na vimelea vya maambukizi ya magonjwa na pia kemikali hizo zina uwezo wa kubadili au kuiga utendaji kazi wa dutu nyingine za mwili  jambo ambalo jambo linalofanya kitunguu saumu kuwa moja ya mitishamba bora zaidi katika kutibu matatizo mbalimbali ya afya

*Nguvu ya kutibu ya Kitunguu saumu inatokana na kuwa na kemikali tiba zifuatazo*
1- Allicin
2- Alliin
3- Alliinase
4- Scordinins
5- Selenium
6- Vitamins(A,B,C and E)
- Kitunguu swaumu ni jamii ya vitunguu ambayo kwa kitaaluma, huitwa *ALLIUM SATIVUM*

- Jamii hii ilianza kutumika katika mabara mbalimbali duniani hususani Asia, Afrika na Ulaya takribani miaka 6000 iliyopita

- Matumizi makuu nyakati hizo yakiwa viungo katika mboga na tiba

- Kitunguu swaumu kimetajwa kwenye vitabu mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika kutibu maradhi mbalimbali yasababishwayo na bakteria, matatizo katika mapafu, matatizo katika mfumo wa umeng’enyaji chakula, na matatizo ya kuishiwa nguvu

- Hakikisha kila mboga unayopika haikosi kitunguu swaumu ndani yake na ikibidi ukiweke mwishoni mwishoni unapokaribia kuepua mboga yako toka katika moto kwamba kisiive sana hata kupoteza viinilishe vyake na ndio maana tunatakiwa Sana kula sosi ya Kitunguu swaumu kilichosagwa bila kuchanganywa na kitu chochote kile

- Lakini ili upate faida zaidi za kitunguu swaumu utatakiwa ukimeze katika maji au ukichanganye na mtindi kikiwa kibichi, yaani bila kupitishwa katika moto au kuwa kimepikwa

- Chukuwa kitunguu swaumu kimoja Kigawanyishe katika punje punje 6

- Menya punje moja baada ya nyingine
Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo sana na kisu na uache hivyo katika hewa kwa dakika 10

- Meza kama unavyomeza dawa na maji nusu lita kila unapoenda kulala

- Namna nyingine nzuri zaidi ni kuviweka ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi freshi koroga vizuri na unywe na hii itakusaidia kupunguza harufu mbaya ya kitunguu swaumu huku ukipata faida nyingine mhimu zilizomo kwenye mtindi

- Fanya hivi kila siku au kila mara unapopata nafasi na hivyo utakuwa mbali na kuuguwauguwa hovyo

*Haya ni baadhi ya magonjwa yaliyothibitika kutibika na yanatibika au kukingika na kitunguu swaumu*
1- Huondoa sumu mwilini, Husafisha tumbo, Huyeyusha mafuta mwilini (Cholestrol)

2- Husafisha njia ya mkojo na kutibu U.T.I, Hutibu amoeba, minyoo na Bakteria wengine

3- Huzuia kuhara damu (Dysentry), Huondoa Gesi tumboni, Hutibu msokoto wa tumbo, Hutibu Typhoid, Huondoa mabaka mabaka kwenye ngozi

4- Hutibu mafua na malaria, Huzuia meno kung’ooka na kutuliza maumivu, Huongeza SANA nguvu za kiume pia hutibu uanithi (kushindwa kusimama kabisa uume)

5- Hutibu maumivu ya kichwa, Hutibu kizunguzungu, Hutibu shinikizo la juu la damu, Huzuia saratani/kansa, Hutibu maumivu ya jongo/gout, Huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula

6- Huongeza hamu ya kula, Huzuia damu kuganda, Husaidia kutibu kisukari, Husaidia kutibu tatizo la kukosa usingizi (ni kweli, na ni moja ya kazi nyingine ya kitunguu swaumu iliyonishangaza zaidi) pia kinaondoa msongo wa mawazo/stress na kukufanya uishi miaka mingi

7- Sifa kuu za kitunguu swaumu ni kuwa na uwezo na faida zilizoainishwa hapo juu ni pamoja kuwa na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti

*Uwezo wake wa kiutendaji unatokana na mambo yafuatayo*
1- Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu

2- Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na kupunguza madhara ya kisukari

3- Iwapo vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bateria, na phytoncide ambayo huua fangasi wa aina mbalimbali

4- Harufu mbaya ya kitunguuu swaumu hutokana na gesi aina ya hydrogen sulfide ambayo hutolewa baada ya kuvila

5- Mama mjamzito chini ya miezi 4 ni vema asitumie vitunguu swaumu kwani vinaweza kusababisha madhara

- LAKINI PIA UWEPO WA KEMIKALI YA *ALLIUM SATIVUM* Katika Kitunguu swaumu kunafanya kitunguu saumu kuwa na uwezo wa kutibu matatizo mengine Kama ifuatavyo:-

1- Kutibu na kukukinga na magonjwa ya mfumo wa upumuaji- magonjwa kama mafua, maumivu ya kifua, kikohozi na asthma haya ni baadhi ya matatizo yanayoweza kutibiwa na kitunguu saumu

2- Kutibu na kupunguza hatari ya magonjwa ya mzunguko wa damu- kitungu saumu kina kemikali ains ya diallyl trisulfide ambayo husaidia moyo kufanya kazi vizuri

3- Kupunguza kiwango cha rehemu mwilini- utafiti uliofanywa na journal of nutritional biochemistry unaonesha matumizi ya kitunguu kwa muda usiopungua miezi 4 unaweza kusaidia kupunguza rehemu(mafuta hatari) ya mwili

4- Kutibu na kuwakinga wanaume dhidi ya saratani ya tezi dume- utafiti uliofanywa na China-japan Friendship hospital na taarifa kuchapishwa katika jarida la asian pacific journal of cancer prevention wa mwaka 2013 unaonesha matumizi ya mimea iliyo na allium ikiwemo kitunguu saumu.kunapunguza hatari ya saratani ya tezi dume kwa wanaume

5- Matatizo ya ini yanayotokana na ulevi uliokithiri- kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Biochimica et biophysica acta inaonesha matumizi ya kitunguu saumu husaidia kutibu matatizo ya ini hasa wale walioathiriwa na pombe

6- Husaidia wanawake ambao huzaa kabla ya wakati wanawake wanaopatwa na matatizo ya kuzaa kabla ya miezi tisa matumizi ya mara kwa mara ya kitunguu saumu hupunguza tatizo hili

7- Huweza kupambana na vimelea vingi vya magonjwa kemikali aina ya allium ndani ya kitungu saumu ina uwezo mkubwa wa kuangamiza vijidudu vya magonjwa vikiwemo vile vya bakteria

8- Husaidia kuulinda mwili dhidi ya saratani hasa ya ubongo kitunguu saumu kina kemikali za organo-sulfur ambazo huangamiza seli zisababishazo saratani

9- Faida nyingine za kitungu saumu ni pamoja na hutumika kutibu kuvu(fangasi) zinazoathiri mwili, Vidonda, Magonjwa ya mfumo wa mkojo kama UTI

*Kitungu saumu hutumikaje kutibu?*
- Sehemu kuu zitumiwazo za kitunguu saumu ni majani na balbu zake(vipande vyake).na huweza kutumiwa kwa namna zifuatazo:-

1- Kutumika kwa kutafuna vipande vyake- vipande vya kitunguu humenya na huliwa kwa kutafuna, tumia vipande walau 7-10 kwa wiki ni wastani mzuri kitiba

2- Kutengeneza juisi ya kitunguu saumu - juisi inayopatikana hutumiwa zaidi kutibu mafua na hutumiwa kwa kijiko kimoja cha chai mara 3 kwa siku tu..!

3- Lulu(maganda mepesi yanayong'aa kabla ya kuvikuta vipande

4- Zina mafuta ambayo huvunwa na ndio yana kiwango kikubwa cha allium

5- Kitunguu saumu huweza kuchanganywa na asali, mchanganyo huu umeonyesha kuwa na matokeo chanya mara dufu ya pale utumiapo kitunguu pekee, pia mchanganyo huu unaonesha kusaidia wanaume wenye matatizo ya nguvu za kiume

6- Mutumizi ya kitunguu saumu kwa watoto chini ya miaka 12 na walishawahi ama wanatumia dawa nyingine za mzunguko wa damu ni hatari kwa afya hivyo basi ni vyema kumuona daktari au mtaalamu wa afya ili upate elimu ya matumizi sahihi ya Kitunguu swaumu kwa Mtoto wako



Hope you enjoy,

Karibu tena, sisi wilnismstore, endelea kutembelea Makala zetu mara kwa mara ili uweze kujifunza mengi

Post a Comment

2 Comments

  1. Dear, kazi nzuri, but badilisha hapo chini, umeandika ili uweze kunifunza badala ya kujifunza

    ReplyDelete
    Replies
    1. 😁😁😁😁😁
      Sawa dear, tayari nishabadili

      Delete
Emoji
(y)
:)
:(
hihi
:-)
:D
=D
:-d
;(
;-(
@-)
:P
:o
:>)
(o)
:p
(p)
:-s
(m)
8-)
:-t
:-b
b-(
:-#
=p~
x-)
(k)