Hivi unaelewa kwamba maneno yako yanaweza kuathiri hisia zako?

Hivi unaelewa kwamba maneno yako yanaweza kuathiri hisia zako?  Mfano kila wakati ukisema maneno kama:-
Naogopa, nimechoka sana, hii ni ngumu sana... Utajisikia hivyo hivyo. Kuna baadhi ya maneno hupaswi kuyasema kabisa! 

Una uwezo wa kujisikia vyovyote utakavyo wakati wowote. Huhitaji jambo kuuubwa litokee ndipo ujisikie vizuri. Unaweza kuamua kujisikia vizuri hata sasa kwa sababu uko hai au tu kwa sababu unataka kujisikia vizuri. 

Amua kuweka mkazo kwa mambo mazuri yanayotokea kwenye maisha yako na uishi kwa matumaini (positive attitude)  kwamba mambo yatakuwa bora zaidi katika siku zako za mbeleni. Ukiwa mtu wa aina hii hisia za udhaifu hazitakuwa na ushindi juu yako


Post a Comment

0 Comments