HAMASIKA, CHUKUA HATUA, BORESHA MAISHA YAKO.


"NANI AMEKWAMBIA HUWEZI?"

Kumekucha,,, Kumekucha,,, Amka nenda kapiganie ndoto zako sasa.
Mtu mmoja mwenye busara sana aliwahi kuulizwa swali kwamba, Kama mtu akikwambia huwezi kufanya jambo fulani, wewe utamjibu na utafanya nini?
"Mtu huyu mwenye busara sana akajibu akisema, Kama mtu akiniambia kwamba siwezi kufanya jambo fulani, kabla sijamjibu lolote, nitajiuliza swali mimi mwenyewe kwamba, Ni kweli siwezi au ni kweli ninaweza, kama jibu langu litakuwa ni kweli ninaweza kufanya jambo hilo basi nitamjibu ninaweza hata kama yeye kasema siwezi, na kama jibu langu litakuwa ni kweli siwezi basi nitamjibu siwezi ili yeye kama anaweza aniambie tunafanyaje."

Loh!!! Umejifunza nini kwa mtu huyu mwenye busara sana? 

Kwanza kabisa ipo hivi, Wewe ndiyo unaejua ukweli wa jambo unalotaka kulifanya, sasa kama unajua ukweli unapata shida wapi?
Kama unaujua ukweli unakwama wapi?

Ina Maana kama ukiwasikia watu wanasema hutaweza, wala huna haja ya kuwachukia au kuwakasirikia, ni swala tu la kujiuliza ikiwa kweli unaweza au huwezi, kama unaweza basi unapuuza maneno yao na unaendelea zako kufanya ili ndiyo uweze sasa lakini kama huwezi unatafuta njia ya kuliweza sasa.

Hamasika, Chukua hatua, Boresha maisha yako.

Uwe na siku njema sana.

Hope you enjoy,

Karibu tena, 

sisi wilnismstore,

Endelea kutembelea Makala zetu mara kwa mara ili uweze kujifunza mengi zaidi

Post a Comment

0 Comments