Tunajua kuwa Yesu ni Mungu katika utatu mtakatifu kutokana kwanza yeye mwenyewe kujifunua kwa kauli zake na maandiko toka kitabu cha Agano la kale.
Yesu alikuwepo toka mwanzo, hata kabla ya kuzaliwa Daudi na Abraham. Mathayo 22:43-45, Yohana 8:56
Atakapokuja huyo roho wa ukweli......yeye atanitukuza Mimi kwakuwa atawajulisheni Yale atakayopata kutoka kwangu. Vyote alinavyo baba ni vyangu. Roho.atawajulisheni Yale atakayo yapata kutoka kwangu. Yohana 15:26, 16:12-15
Yesu akawaambia tena, Amani kwenu! Kama vile baba alivyo nituma Mimi, nami nawatuma nyinyi. Alipokwisha kusema hayo akawaopulizia akawaambia pokeeni Roho Mtakatifu. Yohana 20:21
Na mmeamini kwamba nimetoka kwa Mungu NA sasa nauacha ulimwengu narudi kwa Baba. Yohana 16:27-29
Nimewaambieni mambo hayo kwa mafumbo. Yohana 16:25
Wewe ndiye kristo, mwana wa Mungu aliye hai. Yesu akasema heri wewe Simon kwa maana hakuna binadamu yoyote aliyefunuliwa jambo hili......
Mathayo 16:17
Ikiwa nimewaambieni mambo ya kidunia nanyi hamniamini, mtawezaje kuamini nikiwaambieni mambo ya mbinguni? Hakuna mtu aliyepata kwenda juu mbinguni isipokuwa mwana wa MTU, ambaye ameshuka kutoka mbinguni. Yohana 3:12-13
Mimi Na Baba, tu mmoja!
Yohana 10:30
Baba yuko ndani yangu
na Mimi Niko ndani yake.
Yohana 10:38
Yesu akawaambia nimekaa nanyi muda wote huu, hamjanijua? Aliyekwisha niona mimi amemuona Baba, Mimi Niko ndani ya Baba naye Baba yuko ndani yangu. Mnapaswa kuamini ninaposema Mimi Niko ndani ya Baba naye Baba yuko ndani yangu.
Yohana 14:9-11
Mimi ni ALFA na OMEGA, asema Bwana Mungu kwenye nguvu, aliyeko, aliyekuwako na anayekuja.
Ufunuo wa Yohana 1:8 na 22:12-13
Alfa na Omega - Mwanzo na Mwisho.
-
Maana wajifanya kuwa Mungu Hali wewe ni binadamu tu! Yohana 10:33
Uwe na siku njemaa🙏
0 Comments