SOMO HILI LINA VIPENGELE VITATU.
a. Nini maana ya kufunga
b. Aina za kufunga
c. Mambo ya kuzingatia unapokuwa umefunga
A. NINI MAANA YA KUFUNGA?
MAANA YA KWANZA
–Kufunga kunakoamriwa katika neno la Mungu si kufunga kwa kawaida tu.Asili yake si kukataa chakula ,kujivika nguo za magunia ,na kujitia majivu kichwani .Yeye afungaye kwa kuwa amehuzunishwa moyoni kwa ajiri ya dhambi zake ,Hataki kuonyesha kwa wengine kufunga kwake .
MAANA YA PILI
-Kufunga kule kunakotakiwa kwetu na Mungu ,si kwa kuutesa mwili kwa ajiri ya dhambi rohoni ;Ila kutusaidia kufahamu hali yetu ya dhambi jinsi ilivyo mbaya mno,Ili tujidhili mioyoni mwetu mbele za Mungu na kupokea neema zake na masamaha yake .Aliwaamuru Waisraeli hivi .Rarueni mioyo yenu wala si mavazi yenu mkamrudie Bwana Mungu wenu YOELI 2:13
B. KUNA AINA NNE ZA KUFUNGA AU SAUMU
i. KUFUNGA SIKU MOJA
Ndipo wana Israeli wote, na hao watu wote, wakakwea, wakaenda Betheli, na kulia, wakaketi hapo mbele za Bwana, wakafunga siku hiyo hata jioni; nao wakasongeza sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Bwana waamuzi 20:26, Wakakusanyika huko Mispa, wakateka maji na kuyamimina mbele za Bwana; wakafunga siku ile, wakasema huko, Tumemfanyia Bwana dhambi. Samweli akawaamua wana wa Israeli huko Mispa 1SAMWELI 7:6,
ii. KUFUNGA SIKU TATU
Uende ukawakusanye Wayahudi wote waliopo hapa Shushani, mkafungekwa ajili yangu; msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku wala mchana, nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kisha nitaingia kwa mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie. ESTA 4:16
iii. KUFUNGA SIKU ISHIRINI NA MOJA
Katika siku zile mimi, Danielii, nalikuwa nikiomboleza muda wa majuma matatu kamili. Sikula chakula kitamu, wala nyama wala divai haikuingia kinywani mwangu, wala sikujipaka mafuta kabisa, hata majuma matatu kamili yalipotimia DANIELI 10:2-3
iv. KUFUNGA SIKU AROBAINI
Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi.Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa Mathayo 4:1-2, kutoka 9:9,18, Naye alikuwa huko pamoja na Bwana siku arobaini na masiku yake; hakula chakula, wala hakunywa maji. Naye akaandika katika hizo mbao, hayo maneno ya maagano, hizo amri kumi kutoka 34:28
C. JE MAMBO GANI YAKUZINGATIA UNAPOFUNGA/SAUMU
ISAYA 58:5-10 Je! Kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na Bwana? Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira? e! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe? dipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde.
Ndipo utaita, na Bwana ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu; na kama ukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri.
HAYA NDIYO MAMBO MANNE YA KUZINGATIA.
1. Tahadhali Kutokula chakula kabisa hasa mfungo wa muda mrefu haishauriwi ,kula kiasi kwa ajiri ya afya yako chakula cha kawaida siyo cha anasa kama DANIELI ALIVYOFANYA KATIKA SIKU 21
2. Kufungua vifungo vya uovu,au kuungama dhambi zako zote
3. Kuzilegeza kamba za nira
4. Kuwapa chakula wahitaji katika hili tumia angalau sehemu ya bajeti yako uliyokuwa unatumia kabla haujafunga kuwapa wahitaji au masikini.
JE KUNAFAIDA GANI TUNAZOZIPATA KUTOKANA NA MFUNGO?
1. Utamwita Bwana naye atakuitikia
2. Atakusamehe dhambi zako
3. Utapata afya njema
4. Atakujibu maombi yote uombayo sawasawa na mapenzi ya Mungu.
5. MATHAYO 17:21 {LAKINI NAMNA HII HAITOKI ILA KWA KUSALI NA KUFUNGA}
0 Comments