Kuna Mambo Ambayo Yatayafanya Maisha Yako Yawe Na Thamani Hapa Duniani, Na Kukufanya Uache Alama [Legacy] Ukimaliza Muda Wako Wa Kuishi, Lakini Pia Yatapelekea Upate TAJI Mbinguni, Miongoni mwa mambo hayo ni kama ifuatavyo;
1.WAPE WATU YESU; WAPE HABARI NJEMA ZA MSALABA NA NGUVU YAKE!
-Dunia Imejaa "DHIKI, MAUMIVU, MATESO, HUZUNI, MASIKITIKO NA KILA NAMNA YA UBAYA" Bila "YESU NDANI YAKO KATIKA UKAMILIFU WOTE" Maisha Ni Uwanja Wa Vilio, Majuto, Kutowezekana, Kukosa Utoshelevu, Maumivu Na Mahali Pa Kuchosha.... HII YOTE IKIWA NI MATOKEO YA SHETANI KUWA "mungu wa dunia hii": Na Unaweza Kuishi Juu Ya Shetani na Kila Baya Lake Endapo "YESU AMEJAA NA KUUMBIKA NDANI YAKO" Kiasi Cha Kuweza Kusema, "SHETANI NA KILA SHAMBULIO LAKE HAVINA KITU KWANGU"... Unapompa Mtu Mwingine "HABARI NJEMA ZA YESU" Unakuwa Umempa "NGUVU YA KUUSHINDA ULIMWENGU" Na Akikubali "KUMPOKEA" Anapokea "UWEZO HUO WA KUWA MTOTO WA MUNGU" Ambao Unamfanya "AUSHINDE ULIMWENGU" Maana "KILA ALIYEZALIWA NA MUNGU HUUSHINDA ULIMWENGU"
Watu Wote Ambao "WAMEYATOA MAISHA YAO KWA AJILI YA YESU NA KAZI YA INJILI, NI WATU AMBAO WANAHESHIMA SASA [ACHILIA MANENO MABAYA WANAYOSEMWA NYAKATI FULANI ZA MAISHA WAO NA HUDUMA ZAO] NA HATA WAKIONDOKA DUNIANI, KUMBUKUMBU YAO INABAKI DAIMA"
2.WAPE WATU MUDA WAKO
Unajua Watu Wanahitaji MUDA WAKO KULIKO PESA YAKO... Ukiwa Nao Kwenye Magumu Yao, Changamoto Zao Kwa MANENO YA IMANI, FARAJA NA KUINUA MIOYO YAO, PAMOJA NA KUWAOMBEA, Inaacha Alama Maishani Mwao Kuhusu Wewe Na Maisha Yako... Yesu Alikuwa Na Muda Wa KUWATEMBELEA WAFUATAO: WATOZA USHURU, MAKAHABA, WAGONJWA, WALIOFIWA, MASIKINI, MATAJIRI, WALIOTENGWA NA WATU, WANAOTESWA NA KUONEWA NA IBILISI... Na Maisha Ya Yesu Yameacha Alama Isiyoweza Kufutika Milele!
3.ONESHA UPENDO KWA VITENDO
Watu Walioleata Mapinduzi Ni Watu Ambao WALIONESHA UPENDO WAO KWA VITENDO... Hawakuishia "KUSEMA KUHUSU UPENDO KWA MANENO" Bali Walitoka Na "KUTENDA UPENDO KWA VITENDO"... Mwenye Kanzu Mbili Alimpa Asiye Na Kanzu, Aliye Na Chakula Milo Miwili Alimpa Yule Asiye Na Chakula, Aliye Na Ndugu Wengi Alionesha Upendo Kwa Kuwa Ndugu Wa Wale Wasio Na Ndugu, Aliye Na Vingi ALITUMIA VINGI KUGUSA WENGINE NA VICHACHE KWA AJILI YAKE... Aliye Na Maarifa, Ufahamu Na Hekima Katika Mambo Fulani "HAKUWA MBINAFSI" Ili Aonekane Ya Kwamba Yeye Ndiye "KICHWA AU KILA KITU" Bali ALIHAKIKISHA WENGINE WOTE WAJUE NA KUPATA KILE ALICHONACHO; Na Mwisho Wa Siku Aliacha URITHI USIOFUTIKA!
4.FURAHIA NA LIPA GHARAMA KUWA SULUHU KWA MAISHA YA MWINGINE
Watu Wote Wakuu, Walioacha Alama Isiyofutika Ni Watu Ambao HAWAKUPATA USINGIZI MPAKA WAPATE SULUHU YA MAISHA YA MTU MWINGINE AMBAYE ANAUMIA NA KUTESEKA... Walikuwa Ni Watu WALIOISHI KWA AJILI YA WENGINE!
Kila Mhubiri Mkubwa "ALIYETUMIWA NA MUNGU" Kwa Ishara, Miujiza, Na Maajabu, Alichukua UAMUZI MGUMU WA KUJITENGA NA DUNIA [Marafiki, Vipaumbele Vyake, Anasa, Starehe, Vyakula, Kupoteza Heshima Mbele Ya Watu], KUUTESA MWILI WAKE KWA KUSHINDA AMEJIFUNGIA KUTWA NZIMA NA BIBLIA, VITABU, MAOMBI NA MACHOZI KWA AJILI YA WANAOTESEKA, AU KULALA MILIMANI, KUWEKA KAMBI KANISANI MIEZI KADHAA, Lakini Yote Haya Waliyatenda KULIPA GHARAMA KWA AJILI YA MGONJWA YULE, KIWETE YULE, KIPOFU YULE, KIZIWI YULE NA YULE ALIYEONEWA NA ADUI APATE UHURU... Walikuwa Tayari Hata Kufa Lakini Hawakuacha Kutafuta Suluhu Kwa Ajili Ya Wengine!
Wale Wamilki Wa Makampuni Makubwa, Miradi Mikubwa Ambao WAMEAJIRI MAMIA, MAELFU, MALAKI YA WATU "WALILIPA GHARAMA" Na Kujitesa Ili Wapate Suluhu Kwa Ajili Ya "WASOMI WALIOPATA VYETI LAKINI HAWANA AJIRA WALA UBUNIFU WA KUTUMIA ELIMU YAO KULETA SULUHU" Pamoja Na KUFIKISHA HUDUMA AU BIDHAA KWA WANANCHI WENYE UHITAJI.
Haya Ndo Maisha, Mchezo Rahisi Wa Kanuni.
0 Comments