TAARIFA KWA UMMA KUKAMILIKA KWA AWAMU YA KWANZA NA KUFUNGULIWA KWA AWAMU YA PILI YA UDAHILI WA SHAHADA YA KWANZA KWA MWAKA WA MASOMO 2020/2021


Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inapenda kufahamisha umma na wadau 
wote wa Elimu ya Juu nchini kuwa awamu ya kwanza ya udahili kwa ngazi ya 
Shahada ya Kwanza katika Taasisi za Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 
2020/2021 imekamilika. Majina ya waliodahiliwa katika awamu hii yanatangazwa 
na vyuo husika. 
Katika Awamu hii ya Kwanza ya udahili kwa mwaka wa masomo 2020/2021, 
jumla ya waombaji 90,572 wametuma maombi ya kujiunga katika vyuo 74
vilivyoidhinishwa kudahili. Aidha, jumla ya programu 686 zimeruhusiwa kudahili 
ikilinganishwa na programu 645 mwaka 2019/2020. Vilevile kwa upande wa 
nafasi, mwaka huu kuna jumla ya nafasi 157,770 ikilinganishwa na nafasi 
149,809 mwaka uliopita. Hili ni ongezeko la nafasi 7,961 za Shahada ya Kwanza 
sawa na asilimia 5.3.
Pia katika Awamu hii ya Kwanza ya udahili, jumla ya waombaji 60,621 sawa na 
asilimia 69.9 ya waombaji walioomba udahili wameshapata udahili vyuoni. 
Mwenendo wa udahili wa Awamu ya Kwanza kwa kipindi cha miaka mitatu 
(2018/2019 hadi 2020/2021) unaonesha ongezeko kubwa la waombaji ikiashiria 
ongezeko la wahitimu wa Kidato cha Sita na wale wa Stashahada. Mchanganuo 
wa mwenendo wa udahili kwa Awamu za Kwanza kwa kipindi cha miaka mitatu 
umeainishwa katika Jedwali Na.1.(jedwali katika pdf)





Andika comment yako hapa

Post a Comment

0 Comments