Matatizo ni sehemu ya maisha
Mateso ni changamoto za kuishi
Uvumilivu ni mambo ya kuja na kupotea
Binadamu wengine hawana rizki wanatafuta kwa udi na uvumba wanakosa
Leo hii una uwezo wa kula vipindi vitatu unalalama?
Kuna wenzetu wametafuta watoto kwa hali na mali wakakosa hawajamtoa Mungu makosa leo hii mwaka tu huna mtoto unalalama unasema unaonewa
Kuna wenzetu hata rizki hawana wanaitafuta kwa nguvu zote lakini bidii haifulii wanakosa
Leo hii una uwezo wa kununua dera la msomali unalalama?
Lini tutaweza kukaa chini na kushukuru?
Lini tutampa MUNGU shukran kazi yetu kulalama magari majumba mazuri na maisha mazuri leo hii hio pumzi ikitoweka utakuwa na cha kulalama
Tujifunzeni kushukuru pata kidogo shukuru hata ukikosa usikufuru.
Siku zote, ua lililopo bustanini hua halifikirii kushindana na Ua lenzake lililopo jirani
Yote huchanua. Usijihisi vibaya endapo utakataliwa
Siku zote watu huacha vitu vyenye thamani kwa sababu wameshindwa kuvi-afford.
Kama umefanya makosa, inamaanisha kuna nafasi ya kurekebisha na kuanza upya. Sijui ufunguo wa mafanikio ni upi, ila ufunguo wa kufeli ni kum-please kila mtu na kukubali kuwa mtumwa wa mawazo yake.
Kiwango cha juu cha hekima ni kuishi sasa, kupanga ya baadae na kufaidika na jana yako. Nimejifunza kwamba, mtu jasiri sio yule asiyeogopa lolote, bali ni yule anayeushinda uoga wake ikiwa ni pamoja na kufanya maamuzi magumu.
Naam, maamuzi magumu yenye tija katika maisha
0 Comments